NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii
Josephat Hasunga, amesema serikali haitawavumulia wafugaji watakaobainika
kuingiza Mifugo katika Mapori ya Akiba na Hifadhi za Wanayamapori.
Amewataka na wale wanaoendelea kuingiza mifugo
katika hifadhihi hizo kuacha mara moja na kuondoka katika maeneo hayo, kwani
kuingiza mifugo hiyo katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi ni
ukiukwaji wa sheria za nchi.
Alitoa kauli hiyo akiwa katika
ziara mkoani Morogoro,na baada kupata
wasaa wa kufanya kikao cha pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya usimamizi wa
Wanyamapori nchini (TAWA).
Hasunga aliitaka mamlaka ya usimamizi wa
Wanyamapori nchini, kuboresha miundombinu na vifaa mbalimbali vinavyotumika
katika kupambana na ujangili, ili kuweza kupunguza na kudhibiti matukio hayo.
Kaimu Mkurungezi wa Mamlaka hiyo, Dr
James Wakibara, aalisema wameweka mikakati ya kupambana na kudhibiti ujangili
katika mapori yote ya akiba nchini,na kuwataka wananchi kuacha kufanya uharamia
wa wanayama katika hifadhi yoyote.
“tutambue kuwa kuvamia hifadhi ya akiba
ni kosa,nivyo yeyote atakayekamtwa akifanya ujangili ndani ya hifadhi
atachukuliwa hatua kali za kiseria,wananchi tuwe walinzi wa hifadhi zetu za
taifa,tusikubali watu wachache wakapoteza vivituo vyetu.”Alisema.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment