DOKTA
Shukuru kawambwa akiwapa pole wanakijiji wa ruvu darajani baada ya nyumba zao
kuezuliwa na upepo siku ya tarehe 8 mwezi huu huko katika kata ya vigwaza
wilayani bagamoyo.
Dokta Shukuru Kawambwa akipewa maelezo ya
namna nyumba ya Magdarena Kenya (pichani ) iilvyoezuliwa paa wakati bibi huyo
akiwa ndani ya nyumba hiyo na familia yake na paa hilo kutupwa juu ya mti ulio
jirani huko katika kijiji cha ruvu darajani kata ya vigwaza wilayani bagamoyo.
Dokta Shukuru Kawambwa akimpa pole Salome baaada
ya nyumba yake kuezuliwa na upepo,ambapo
yeye na familia yake kukosa makazi huko katika kijiji cha ruvu darajani kata ya
vigwaza wilayani Bagamoyo.
JUMLA
ya nyumba 65 zimeezuliwa kwa upepo ulioambatana na mvua kubwa na kusababisha
baadhi ya kaya kukosa makazi katika vijiji vya ruvu darajani na visezi kata ya
vigwaza wilayani bagamoyo mkoani Pwani.
Hayo
yamebainishwa baada mbunge wajimbo hilo na waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi
docta shukuru kawambwa wakati alipofanya ziara ya siku moja kutembelea vijiji
hivyo kujionea hali halisi ya ajali hiyo ya mvua iliyoambatana na upepo mkubwa.
Dokta
Kawambwa amesema tukio hilo lilitokea novemba 8 mwaka huu majira ya kati ya saa
5 hadi saa 7:30 mchana ambapo vitongoji vilivyo athiriwa na upepo na mvua hiyo
kuwa ni pamoja na mlimani,mwegeyani na mkuwajuni ambapo katika nyumba hizo 65
ni pamoja na nyumba mbili za ibada yaani makanisa ya RC na kanisa la
kipentekoste.
Amesema
kati ya nyumba hizo nyumba 23 zimeezuliwa kabisa mapaa yake na nyumba 42
zimeezuliwa na kubomoka upande mmoja wa mapaa yake ambapo docta KAWAMBWA
alipata nafasi ya kutembelea na kukagua uharibifu uliotokea na kuwapa pole
waathirika wa ajali hiyo.
Dokta
Kawambwa ameahidi kupeleka viloba 67 vya
unga na mchele hukuakiomba wadau mbalimba;li na wasamalia wema kujtolea
kuwasaidia wananchi wa vijiji hivyo vya ruvu darajani na visezi kwa hali na
mali kuwanusulu na mahafa yaliyowakuta na kuagiza msaada huo wapewekipaumbele zaidiwalioathirika
zaidi, wazee, wasio na uwezo kabisa .
Ameagiza
uongozi wa vijiji hivyo na kata ya vigwaza kupeleka taarifa za kimaandishi
haraka katika ofisi ya wilaya ya bagamoyo hatimaye taarifa rasmi zifike mkoani
hadi ofisi ya waziri mkuu kitengo cha maafa ili hatua zaidi za kimsaada
zichukuliwe.
No comments:
Post a Comment