Matukio kadhaa ya migogoro ya ardhi katika
wilaya ya Kilosa yamesababisha vifo vya raia , waathirika wengi wakiwa ni
wanawake na watoto ambao wanakuwa tegemezi kubwa katika jamiii katika suala
zima la uzalishaji katika kilimo na ufugaji
Mratibu
wa muungano wa asasi, zilizopo mkoani
Morogoro zinazohusika na maswala ya
ardhi (Morogoro
Land Allliance),Julius Mabagala anasema kuwa taasisis yao ilifanya utafiti wa
migogoro ya ardhi katika makundi tofauti katika wilaya ya Kilosa yakiwemo kundi la viongozi wa vijiji,
wakulima na wafugaji kwa lengo la kutafuta chanzo cha migogoro na nini
kifanyike
Katika
utafiti waligundua kuwa kuna aina nyingi za migogoro ya ardhi inayosababisha
jamii kukosa amani kila siku na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo ambayo
ni mipaka kati ya ardhi ya vijiji,wafugaji na wakulima,wakulima na wakulima
katika mipaka ya mashamba
Migogoro
mingine ni kati ya wananchi wazawa na wawekezaji,wanachi na serikali hasa mbuga
za wanayama,hifadhi za taifa,na mtu na mtu katika makazi,ukodishaji
ardhi,miradhi ya mashamba ni baadhi ya vitu ambavyo vinachangia vurugu katika
jamii nyingi za wazalishaji ndani ya Taifa kwa ujumla
Mabagala
anasema kuwa vyanzo migogoro ya ardhi ni utawala na uongozi ambapo viongozi
wengi wanafanya maamuzi yasiyo na kumbukumbu,viongozi wasiowajibika kutokana na
maamuzi au vitendo vya masuala ya ardhi,viongozi kutumia madaraka viabaya kwa
manufaa yao binafsi na kuongeza mipaka bila kufuata taratibu na sheria ya
umiliki wa ardhi ngazi ya kijiji
Anasema migogoro mingine
inasababishwa na wakulima na wafugaji wenyewe katika kuwepo
kwa mifugo mingi kuzidi uwezo wa eneo lililotengwa,kutenga maeneo ya malisho
bila kujali idadi ya mifugo iliyopo,wafugaji kutotii taratibu na sheria
zilizowekwa,wakulima kuvamia maeneo ya wafugaji na kuanzisha shughuli za
kilimo,elimu duni ya sheria ya ardhi kuhusu matumizi bora ya ardhi na wakulima
na wafugaji katika mipaka ya mashamba
Taasisi ilipendekeza mambo mbalimbali kama yafuatayo kama vili
kijiji kipimwe au mipaka ihakikiwe ili kutambulisha eneo na Miliki ya ardhi ya
kijiji kisheria,kuwepo na mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji,kuwepo
alama za kudumu ili kubainisha Mipaka
ndani ya maeneo ya mpango wa matumizi wa ardhi ya kijiji,Wananchi wamilikishwe
ardhi kwa hati za kimila na kuwepo na masijala ya ardhi ya kijiji ili kuweka na
kutunza kumbukumbu za masuala ya ardhi
Mapendekezo
mengine ni wananchi waelimishwe taratibu za kusuluhisha au kutatua migogoro
ya ardhi kwa uwazi na haki,kamati zote
zinazohusika na masuala ya ardhi kijijini zipewe elimu ya kutosha ya sheria ya
ardhi na vitendea kazi vyake ili kamati zizingatie taratibu na kutoa haki na wajumbe
wa kamati zote wachaguliwe katika mkutano wa wananchi wote kwa kufuata taratibu
za kisheria zilizopo ili kuepuka chochoko ya vurugu
Mbagala
anasema kuwa hatua stahiki za ufumbuzi wa
migogoro ya ardhi ya vijiji ni,kuwapatia wafugaji wenye idadi
kubwa ya mifugo maeneo yenye malisho na maji ya kutosha vijijini,kuwepo mpango
wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji,serikali kuwapati ranchi ndogo ndogo
wafugaji wenye idadi kubwa ya mifugo,wafugji waunde chombo cha sauti ya
wafugaji katika maeneo yenye migogoro ya ardhi
Hatua nyingine ni serikali
itunge sheria ndogo zinazothibiti uhamiaji horera wa wafugaji, serikali na
vijiji ziweke utaratibu wa kuhesabu na
kuthibiti idadi ya mifugo katika vijiji na wilaya kila mwaka,kuwepo na
utaratibu wa wazi wa kuwajibisha viongozi wanaokiuka sheria na taratibu za
uhamiaji wa wafugaji vijijini na wilayani na serikali itunge sheria ya wafugaji
kumiliki ardhi kimila.
Katika
ripoti ya warsha ya maafisa ardhi wa sekretarieti za
mikoa
na makatibu tawala wa wilaya (das) juu ya migogoro ya mipaka na ardhi nchini
iliyofanyika tarehe 12-13 april 2006 mjini Morogoro iliainisha changamoto
mbalimbali zilizopo katika migogoro ya ardhi
Ilibainisha
changamoto hizo kuwa ni uwezo wa mabaraza ya ardhi ya Wilaya/ kata na Kijiji ni
mdogo na pia maamuzi yanayotolewa hayapati nguvu za dola ili yatekelezeke na
hivyo kufanya migogoro ya mipaka na ardhi izidi kukua.
Upungufu
wa Wataalamu wa kada ya Ardhi katika ofisi za Wilaya,hii ni pamoja na ukosefu
wa majengo mazuri ya ofisi, fedha za kuendeshea ofisi, vifaa vya utendajikazi
kama GPS, Total station, vifaa mbalimbali vya kuandaa ramani
pamoaja
na usafiri kwenye Idara za Ardhi na kufanya kazi ya kutembelea mipaka kuwa ni
ngumu sana.
Changamoto
nyingine ni wanasiasa kuingilia sana maamuzi ya wataalamu wa ardhi kwenye kutoa
maamuzi ya migogoro ya ardhi na mipaka na kusababisha migogoro hii kukua au
kutopatikana kwa ufumbuzi kwa wakati unaotakiwa na wananchi kuendelea kupoteza
mali zao
Nyingine
ni viongozi wa mikoa na Wilaya kutoifahamu mipaka ya maeneo yao ya kiutawala na
kusisitiza viongozi wa mikoa na wilaya wanapoteuliwa ni muhimu watembelee na
kufahamu kwa uhakika mipaka ya maeneo yao ya utawala.
Wataalamu,
watendaji na viongozi hawazifahamu kwa uzuri sheria za ardhi na
kupendekezwa kwamba nilazima wasome na
kujua sheria zote za ardhi zinazozungumzia utatuzi wa migogoro hiyo na halmashauri
ziwajibike mara moja mgogoro wa ardhi unapojitokeza, ili kuzuia mlundikano wa
migogoro ambayo hatimaye huwa kero kubwa kwa wananchi.
Mashamba
yaliyotelekezwa yafutiwe hati za umiliki mara moja na Wizara ya Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi ichukuwe hatua za haraka mara tu maombi mapya
yanapowafikia.
Maeneo
yaliyobinafsishwa wakati wanakijiji wakiwemo ndani yaangaliwe upya kwani
wanakijiji waliokuwa ndani wanapata matatizo pamoja na kuimarishwa kwa
mawasiliano kuanzia ngazi ya Wizara zote husika, Mikoa na Wilaya na kuwa na
mrejesho ya taarifa husika ili kuwafnya wanachi kuwa na imani na viongozi wanaowaongoza.
Kwa upande wake mkulima Lamanya Mdoe anasema kuwa migogoro ya wakulima na wafugaji morogoro imeanza muda mrefu sana ila tatizo kubwa linakuwa kwa watendaji kuanzia serikali za vijiji hadi mkoa
Mdoe anasema kuwa waziri husika imefika wakat isasa kuchukua hatua kwa watendaji wote wanaohusika katika sakati zima la kuuza ardhi kwa maslahi binafsi bila kushirikisha wanakijiji kama sheria ya ardhi inavyoelekeza na kuwachukulia hatua za kisheria ili wengine kuweza kuiga na kuacha tabia hiyo yakuzorotesha maendeleo katika jamii
Mwisho..........................
Mdoe anasema kuwa waziri husika imefika wakat isasa kuchukua hatua kwa watendaji wote wanaohusika katika sakati zima la kuuza ardhi kwa maslahi binafsi bila kushirikisha wanakijiji kama sheria ya ardhi inavyoelekeza na kuwachukulia hatua za kisheria ili wengine kuweza kuiga na kuacha tabia hiyo yakuzorotesha maendeleo katika jamii
Mwisho..........................
No comments:
Post a Comment