Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kilombero Abdul
Daraja la muda linalotumiwa na mafundi wanaojenga daraja la mto Kilombero kuvusha vifaa,daraja hilo ndilo alilopita Rais Kikwete akitokea Ulanga kuelekea Ifakara.
Daraja la muda la mto Kilombero linavyoonekana kwa juu. |
RAIS Jakaya
Mrisho Kikwete amesema serikali imedhamiria kukamilisha ujenzi wa daraja la mto
Kilombero kwa wakati kwa lengo la kurahisisha huduma kwa wananchi wa Ulanga na
Ifakara na kuweka lami kwa baadhi ya barabara
kubwa zinzounganisha wilaya hizo na kutatua kero wanayoipata kipindi cha
mvua.
Kikwete
alitoa kauli hiyo jana akiwa katika zoezi la kuweka jiwe la msingi katika ujenzi
wa daraja la mto Kilombero,ambapo alisema kuwa serikali katika mpango wa
maendeleo katika kipindi cha awamu ya tatu ilidhamiria kujenda madaraja matatu
ambayo ni Kilombero,Kigamboni na Malagarasi
Alisema kuwa
ujenzi wa daraja la kigamboni utakamilika ifikapo mwezi wa 6,2015 kwa ni
jitihada zinaendelea zinaonekana na kuweza kupunguza adha ya wakazi wa
kigamboni wanayoipata kwa kipindi hiki kifupi katika kufanya shughuli zao za
maendeleo
Aliongeza
kuwa katika kipindi ch 2005/2010 serikali iliahidi kurekebisha miundo mbinu ya
barabara kwa kutimiza ilani ya chama cha mapinduzi , kuna wengine walisema ni
ahadi hewa zinatolewa ila kwa sasa wanashuhudia wenyewe maendeleo yaliyoletwa
na bado serikali ina mpango wa kuhakikisha barabra zote zinapitika kwa kiwango
cha lami
Pia alisema
barabara ya kutoka Ruaha hadi Ifakara itajengwa kwa kiwango cha lami,kwani
wasanifu wameshaanza kazi na pindi watakapomaliza ujenzi huo utaanza,na
Barabara ya Kilombero mpaka Mahenge,Ifakara,Mgeta na Mlimba zitaingizwa katika
ilani ijayo ya chama cha mapinduzi
Kwa upande
wake Waziri wa Ujenzi,John Pombe Maguli alisema kuwa kukamilka kwa daraja la
mto kilombero kutafanya mji wa ifakara kuwa na maendeleo ya hali ya juu na wa
kisasa kwani kila kitu kitakuwa kinapatikana mji hapo na kwa urahisi kuliko
ilivyo sasa
Magufuli
alisema daraja la kilombero lina urefu wa mita 384 na upana wa mita 120,huku
kukiwa na madaraja mengine madogo madogo 35,pia daraja hilo linajengwa kwa
kiwango cha kimataifa kinakidhi vigezo vyote
vinavyotakiwa vya ujenzi wa madaraja
Alisema kuwa
serikali itaendelea kuhakikisha mkandarasi anafanya kazi kwa makini na
kukamilisha daraja hilo kwa wakati na kuhakikisha analipwa malipo yake wa
wakati kama walivyokubaliana katika mkataba waliosaini ili kusiwe na sababu za
kuchelewesha malipo hivyo daraja kushindwa kukamilika katika ubora unaotakiwa.
Naye Afisa
Mtendaji Mkuu kutoka wizara ya Ujenzi ,Mhandisi Francis Mfugale alisema kuwa ujenzi
wa daraja hilo ambao utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 53.2,asilimia 90 ya
mitambo yote imekamilika na kufikishwa
katika eneo la ujenzi baada ya kufanyiwa tathimini nchini china wakishirikiana
na watanzania waliokwenda huko.
Mfugale
alisema kuwa ujenzi wa daraja hilo umechelewa kuanza kutokana na mafuriko,baada
ya mafuriko wataalamu walikaa na kutathimini aina gani ya daraja watengeneze
ambalo litakuwa suluhisho ya adha ya usafiri wanayopata wakazi wa Ifakara na Ulanga
kipindi cha mvua kubwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment