Mhandisi wa Mamlaka ya Maji Bonde la Wami/Ruvu,Abdallah Mshana akionyesha wanahabari jinsi wakulima wa mpunga wanavyoharibu kingo mto wami ili kupata maji ya umwagiliaji |
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumiaji maji, John Daniel akitoa maelekezo kwa wanahabari jinsi wakulima wa mpunga wanavyotumia maji bila kuwa na kibali katika kumwagilia mashamba yao. |
Akizungumza baada ya zoezi la upandaji miti liliofanywa na mamlaka ya maji Bonde la Wami Ruvu katika mto mgeta uliopo wilayani mvomero katika vijiji vya Kibaoni na Lukuyu, Mhandisi wa Mazingira Abdallah Mshana alisema kuwa zoezi hilo limefanyika baada ya kuona miti mingi imekatwa na kusababisha wingi wa maji kupungua katika maeneo mbalimbali
Mshana alisema kuwa uharibifu wa mazingira umekuwa ukiongezeka kila siku kutokana na shughuli za kibinadamu za kutafuta mahitaji yao hata sehemu zenye misitu ya asili ambayo kuchangia kuhifadhi maji katika sehemu mbalimbali na wao kukata miti kwa kupasua mbao ama kuchoma mkaa jambo ambalo sio sahihi kufuatana na sheria za utunzani wa mazingira
Alisema kuwa kufuatana na sheria ya utunzaji wa vyanzo vya maji ni mafuruku mtu kufanya shughuli za kilimo katika chini ya mita 60 kutoka katika chanzo cha maji ila wanachi wengi hawataki kufuata sheria hiy na wengine wanadai kutohifahamu kwa lengo la kuendele a kuharibu vyanzo vya majina kusababisha upungufu wa maji
Aliwataka wakazi wa mgeta kutunza miti iliyopandwa na zoezi la upandaji wa miti ni endelevu katika maeneo yote inakopita mito ambayo inamwaga maji katika bonde la wami ruvu hivyo ni wakati wa viongozi wa seriklia za vijiji kushirikiana na wanachi katika kutunza miti hiyo kwani kwa mwananchi ambaye mti umepandwa katika shamaba lake kipindi cha mavuno atafaidika mhusika wa shamba hivyo kujituma katika kutunza mazingira
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Mgeta,Makame Kai,alisema kuwa yeye kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji husika wataunda vikundi mbalimbali kila kijiji vya utunzaji wa mazingira na kuvipa majukumu ya kutunza miti ihyo na utunzaji wa mazingira kwa ujumla kwani wakati mwingine kufanya kazi bila kuwa na vikundi wengine hawajitikezi katika shughuli za kujitolea kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla
Kai alisema kuwa suala la utunzaji wa mazingira linamgusa kila mtu na hivyo ni wajibu wa kila mwanachi kuanza kutunza mazingira kuanzia nyumbani kwake na sio kutegemea serikali ya kijiji ama ya kata na kuwataka viongozi wote kuwa mastari wa mbele katika zoezi hilo na kiongoz iyeyote atayehusika katika uharibifu wa mazzingira atachukuliwa hatua za kisheria
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kibaoni Joseph Hungu alisema wanakabiliwa na chanamoto kubwa ya elimu ya mazungira jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya mgeta na maeneo jirani hasale wale wanaozunguka misitu ya asili na vyanzo vya maji
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mgeta,Makame Kai,akipanda mti kando kando ya mto mgeta katika kijiji cha kibaoni na Lukuyu kwa lengo la kuhifadhi maji ,zoezi lililofanywa na Mamlaka ya maji Bonde la Wami/Ruvu.
No comments:
Post a Comment