Tuesday, March 12, 2013

WAKINA MAMA WAJAWAZITO WATOZWA SH.45,000 WAKATI WAKUJIFUNGUA


WAKINA mama wajawazito kutoka katika kata za Diongoya,Muhonda na Tuliani wilayani Mvomero wanalazimika kujifungulia majumbani kutokana na kutozwa ghalama ya shilingi 45,000 wakati wa kujifungua katika hospitali ya Bwagala.

Wakizungumza na Jambo na Leo,akina mama wa Tuliani walisema kuwa wanalazimika kujifungulia majumbani kwani hawana fedha  ya kujifungua katika hospitali hiyo ambapo walisema wanachofahamu wao ni kwamaba wamama wajawazito wanatakiwa kupata huduma bure.

 Walisema kuwa nashangazwa na watoa huduma  wa hospitali hiyo kuwatoza ghalama hiyo wakati serikali ya Tanzania iliwahi kutangaza kuwa kinamama wajawazito wanatakiwa kujifungua bure bila kutozwa gahalama yeyote.

 “Sisi kama wananchi tunajiuliza ni lini wilaya ya Mvomero itajenga hospitali yake ya wilaya ili kuepuka ghalama kama hizi,kwa sasa tunalazimika kutumia hospitali hii teule ya Bwagala kwani hakuna hospitali nyingine labda twende mjini morogoro,”alisema Abubakar Sengi aliyedai kumpeleka mkewe kujifungua katika hospitali hiyo

 Kwa upande Makame  Kai afisa mtendaji wa kata ya Mgeta wilayani humo akiwa katika hospitali hiyo ambapo alimpeleka mgonjwa wake alisema alipofika katika hospitali hiyo aliambiwa atoe kiasi cha shilingi 45,000 ili mgonjwa wake aweze kupatiwa huduma.

 Kai alisema kuwa ni vyema uongozi wa hospitalli ya Bwagala ukazingatia agizo la serikali la kuhakikisha akinamama wajawazito wanapatiwa huduma zote za msingi wakati wa ujausito wao bure na si kufanya kama alivyojitokeza kwa mgonjwa wake.

No comments:

Post a Comment