Tuesday, August 12, 2014

ELIZABETH TARIMO ATWAA TAJI LA MISS REDDS KANDA YA MASHARIKI.


                                                                           
Miss Redds Kanda ya Mashariki Elizabeth Eliud Tarimo katika akiwa na wenzake baada ya kutangazwa mshindi.
MREMBO Elizabeth Eliud Tarimo(18)kutoka mkoa wa Lindi  ametwa taji la mrembo wa kanda ya mashariki ,kwa kuwashinda washiriki wenzake kumi na moja, sambamba na kujinyakulia kitita cha shilingi laki nne na cheti.

Katika shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Nashera mjini hapa na kuhudhuriwa na watu lukuki akiwemo Mbunge wa Kilosa,mh.Mustafa Mkullo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shindano hilo lililokuwa la kusisimua.

Dalili za Tarimo kunyakua taji hilo lilianza kujionesha tangu mwanzo,wakati wanyange hao kumi na mbili wakipita mbele ya majaji,wakiongozwa na jaji mkuu Hashim Lundenga,ambapo Tarimo alionesha hali ya kujiamini huku muda wote akitabasamu.

Mnyange huyo alinga’ra vilivyo katika vipengele vyote,kuanzia mavazi ya ufukweni,ya mtoko sambamba na kujibu swali kwa uhakika na kujiamini,huku akiwaacha mashabiki wakimshangilia kwa nguvu zote na na kuwafanya majaji kuwa katika wakati mgumu.

Nafasi ya mshindi wapili ilichukuliwa na mnyange Nidah Katunzi aliyejinyakulia kitita cha shilingi laki tatu, ambaye alionesha upinzani mkubwa kwa Tarimo,huku wadau wa urembo wakishindwa kujua nani kati yao anaweza kutwaa taji hilo lililoshirikisha washiriki kutoka mikoa ya Lindi,Morogoro,pwani na Mtwara.

Mnyange Lucy Julius Diyu alifanikiwa kunyakua nafasi ya tatu na kufanikiwa kujinyakulia kitita cha shilingi laki mbili sambamba na cheti ,wakati mshindi wa nne alijinyakulia shilingi laki moja na nusu,huku washiriki wengine waliobaki wakiondoka na kifuta jasho cha shilingi laki moja.
Kwa upnade wake Mbunge wa Kilosa Mustafa Mkulo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kinganganyiro hicho alisema kuwa tasnia ya urembo ni ajira katika jamii hivyo warembo wajitokeze kwa wingi kushiriki katika mashindano hayo
Mkulo alisema kuwa imekuwa ikijengeka katika jamii dhana ya urembo ni uhuni,jambo ambalo sio sahihi kwani kuna watu wengi wamepitia katika tasnia hii na wana maendeleo mazuri na wanaitangaza nchi yetu duniani

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo,Hashim Lundenga ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania ,alisema kadri miaka inavyokwenda ndivyo wanyange wenye weledi mkubwa wanavyojitokeza na hivyo kufanya mashindano kuwa na msisimko zaidi.

Alisema warembo wengi kwa sasa wanaojitokeza wana elimu nzuri ya ngazi ya chuo,hivyo uelewa wao ni mkubwa na rahisi kufundishika ,tofauti na miaka ya nyuma ambapo wasichana wengi waliokuwa wakijitokeza ni kutoka mitaani.

Mwisho

No comments:

Post a Comment