Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera akisalimiana na wachezaji mara baada ya kufungua mshindano ya Airtel Rising mjini Morogoro. |
MKUU wa mkoa wa Morogoro Dk. Joel Nkaya Bendera ameziagiza
timu mbalimbali za mpira wa miguu hapa nchini kuhakikisha zinakuwa na wachezaji
wa akiba kwa kuanzisha vilabu vya vijana wa umri wa chini ya miaka kuanzia 16
ili kukuza mpira Tanzania.
Bendera alisema hayo jana wakati akifungua michezo
wa ligi ya mkoa kwa vijana chini ya miaka 16 yajulikanayo kama Airtel Rising
star yaliyoshirikisha timu za Moro kids, mwere kids na take fort ya Kilombero yaliyoandaliwa
na kudhaminiwa na Kampuni ya simu Airtel hapa nchini.
Bendera alisema, hakuna uchawi katika michezo bali
ni suala la kumuandaa mchezaji tangu akiwa mdogo na kuweza kumuandaa mchezaji
kwa kumuondoa woga na kuwaweka katika hali ya kujiamini.
Alisema kuwa suala la mpira ni lazima mchezaji
afundishwe akiwa na umri mdogo kwani katika umri huo pia ataweza kuona na kujua
vyema mbinu zote za mpira wa miguu.
Akizungumza katika Michezo hiyo Ofisa uhusiano wa
Airtel Jackson Mbando alisema, mashindano hayo kwa sasa yanachezwa katika nchi
zote 17 za Afrika na kufanya kuwa na mashindano ya nchi kwa nchi tofauti na
mwanzoni yalikuwa yakichezwa na kuishia hapahapa nchini.
Alisema kuwa vijana hao wanashindana na baadhi
kuchaguliwa na kuunganishwa na vijana walioandaliwa kutoka mikoa mingine ambapo
watashiriki katika mashindano ya nchi kwa nchi huko Gabon.
Ofisa Masoko wa Airtel kutoka kanda ya Pwani Aminata
Keita alisema kuwa kampuni hiyo huwapa nafasi vijana ya kuonesha na kukuza vipaji
ili kuendeleza soka nchini ambapo kwa mwaka huu wamechukua vijana kuanzia umri
wa miaka 15.
Aliwaomba vijana waweze kujitokeza kwa wingi katika
michezo hiyo kwa miaka ijayo ili kuliinua Taifa kimichezo wakiwemo wasichana na
wavulana ambapo mwaka 2012 wasichana walibuka washindi katika mashindano kama
hayo yaliyofanyika nchini
No comments:
Post a Comment