Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro,Leonad Paul akiwaonyesha wanahabri koti walilokuwa wakitumia majangili |
Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro
Leonard Paulo alisema kuwa tukio la kwanza lilitokea mnamo Julai 16 mwaka huu
majira ya saa 2.30 usiku huko katika eneo la Mzombe Tarafa ya Mikumi katika
Wilaya ya kipolisi Ruhembe Mkoani Morogoro.
Kamanda alisema kuwa askari
waliokuwa katika eneo nla ukaguzi waliwatilia shaka watu wawili waliokuwa
wamevalia makoti meusi,begi pamoja na silaha wakiwa wanaendesha pikipiki
yenye nambari za usajili na T 630 BVH aina ya SUN LG na
walipopekuwaliwa walikutwa wakiwa na silaha aina ya Riffle yenye namba AO 48441
pamoja na risasi 13 ambayo ilikuwa ikitumiwa katika kufanya
ujangili wa kuua wanyama mbugani.
Aliwataja majangili hao kuwa ni
Ayoub Obeid (34) maarufu kama Mkwenjele pamoja na Nassoro Mohamed (34)
maarufu kama Kambala wote wakazi ni wakazi wa Kilosa Mkoani Morogoro.
Alisema kuwa watuhumiwa wamekamatwa
na uchunguzi zaidi unafanywa na jeshi la polisi ili kuweza kubaini mtandao
mzima unaojihusisha na matukio ya ujangili ili sheria ziweze kuchukua mkondo
wake.
Katika mwendelezo wa operesheni hiyo
mnamo juni 13 hadi julai 3 mwaka huu pia jeshi hilo liliweza kuwakamata
watu watatu wanaosaidikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha aina ya AK 47
ikiwa na risasi 3 ambao waliweza kufahamika kuwa ni Said Salehe (30) mkazi wa
kilosa ,Alias Makwawa (30) mkamkazi wa Ludewa Mbuyuni wote wakazi
wa kilosa pamoja na Abdul Mateo maarufu kama baba ubaya (30) mkazi wa Turiani.
Wakati huo huo mnamo Julai 3 mwaka
huu majira ya saa 2.30 katika Wilaya ya kilosa watu wawili wanaosadikiwa kuwa
ni majambazi wakiwa na silaha aina ya gobore likiwa na risasi moja
walijaribu kupora duka la mfanyabiashara na hatimaye kushindwa kuiba
baada ya kubishana na mfanyabishara na kushindwana nguvu na kisha kutoroka
kusikojulika na wanaendelea kusakwa na jeshi hilo.
Kamanda Paulo alisema kuwa
kufanikiwa kukamatwa kwa watu hao ni kutokana na jeshi la polisi kuanzisha
programu maalumu ya operesheni shirikishi ambayo inashirikisha wananchi moja
kwa moja katika kuwafichua wahalifu.
Hata hivyo kamanda huyo ametoa
wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kupitia operesheni hiyo ili
kuweza kufichuwa wahalifu wanaoishi katika maeneo yao ili kukomesha
kabisa vitendo vya uhalifu ndani ya mkoa.
Kamanda Paul akiongea na wanahabari juu ya operesheni shirikishi. |
Baadhi ya askari kanzu wakikagua silaha zilizokamatwa katika zoezi la operesheni tokomeza |
Waandishi wa habari mkoani Morogoro wakimsubiri Kamanda wa Polisi wa mkoa Leonad Paul katika ukumbi mdogo wa polisi |
Kamanda Leonad Paul akionyesha bunduki iliyokuwa inatumiwa na majangili kuua wanyama aina ya tembo na swala. |
Waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda wa polisi wa mkoa wa morogoro Leonad Paul. |
No comments:
Post a Comment