Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Joel
Bendera amewataka maafisa habari katika taasisis na idara mbalimbali za
serikali kutowakimbia waandishi wa habari wanapofika ofisini kuuliza jambo
lolote kwani kufanya hivyo ni kuwanyima wananchi habari na hakuna nchi
inayoweza kuendelea pasipokuwa na vyombo vya habari
Dkt Bendera alisema hayo jana
wakati mkutano wa 98 wa watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma
kupitia Shirika la utangazaji la taifa (TBC) uliofanyika mjini Morogoro na
kufadhiliwa na mfuko wa Pensheni wa PSPF
Alisema kuwa jamii inapaswa kujua
nini kinachofanyika ndani ya nchi yetu,hivyo ni wajibu wa yeyote
aliyepewa mamlaka kushirikiana na wahabari na katika kuhakikisha jamii inapata
elimu mbalimbali kupitia vyombo vya habari na sio kuwakimbia waandishi
Bendera alisema kuwa habari
nyingi zinaandikwa kwa kulenga watu wa mjini na hivyo kuwanyima fursa watu wa
vijijini kupata habari kwa kutotambua kuwa wanakubwa na changamoto nyingi za
kimaisha na zinatakiwa kutambulika katika jamii,pia mafunzo hayo wayatumie
zaidi kuwasaidia watu wasio na sauti
“wananchi wengi wa vijijini
wana kero nyingi sana ambazo hazitambuliki,hivyo vyombo vya habari mutmie fursa
kuandaa vipindi maalumu vinavyo lenga na kuibua kero vijini ili kuweza
kuzipatia ufumbuzio”Alisema Bendera
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni
wa PSPF Adam Mayingu alisema kuwa kuwa ni vyema wananchi waka mstari wa mbele
kujitokeza kujiunga na mfuko huo maalumu unaomwezesha mwanachama kufanya
uchaguzi wa fao analolihitaji kujiunga nalo.
Alisema kuwa PSFP inatoa
mafao mbalimbali ikiwemo fao la uzeeni ,fao la ulemavu,fao la kifo,msaada wa
mazishi ,fao la wategemezi ,fao la uzazi ,fao la kufukuzwa kazi na mengineyo
ambapo mpaka sasa mfuko huo umeweza kuhudumia wanachama na wategemezi zaidi ya
400,000.
Mayingu alisema kuwa mbali na mfuko
huo kutoa mafao mbambali pia umeweza kuhakikisha wastaafu wanaendelea kupata
maisha bora kwa kuslipwa mikopo maalumu kwa wastaafu kwa kushirikiana na
benki ya posta Tanzania ambapo imezindua mikopo maalumu kwa wastaafu hao
Mkurugenzi wa Shirika la Utangzaji
Tanzania(TBC) Clement Mshana alisema kuwa mafunzo hayo yawawezesha watarishaji
na wahariri wa vipindi vy redio na televisheni kuwa chachu kwa kutengeneza
vipindi vitakavyokuwa dira ya maendeleo kwa wananchi ambao wanategemea vyombo
vya habari katika mabadiliko makumbwa ya maendeleo duniani
Hata hivyo katika mafunzo hyo Mkuu
wa Mkuo wa Morogoro Dkt. Joel Bendera aliweza kujiunga rasmi kujiunga na
mfuko huo wa hiari na kuwataka wananchi kujiunga na mfuko huo ili kuweza
kunufaika kwa sasa na hata kipindi cha uzeeni.
No comments:
Post a Comment