Wadua wakifuatilia mada. |
Meya wa Manispaa ya Morogoro,Amir Nondo akitoa neno katika mkutano huo. |
Viongozi wa serikali wakifuatilia jambo katika mkutano. |
Wadau wakifuatilia mada,wa kwanza ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro Gervis Sembey |
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera akifungua mkutano huo uliofanyika katika hotel ya Glonency. |
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera,Meya wa Manispaa ya Morogoro katika Amir Nondo wakiwa katika matembezi nje ya ukumbi. |
Akifungua
mkutano wa wadau wa mfuko wa bima ya Afya na mfuko wa jamii,Bendera alisema
kuwa viongozi wa serikali lazima kuwa mstari wa mbele katika kujiunga na kutoa
elimu ya mfuko wa bima ya afya katika jamii wanazosimamia kila wakati kwani
afya ni uhia wa kila binadamu
Bebdera
alisema viongozi na watoa huduma ya mfuko wa afya wanapaswa kujifunza kwa
wengine ambao wamefanikiwa wametumia mbinu gani ili na mkoa wa morogoro kuwa
mfano wa kuigwa katika zoezi zima la kutekeleza zoezi zima la kujiunga na mfuko
huo ili kuapata huduma za uhakika pindi wanapopata matatizo ya kiafya
Aliwataka
watoa huduma katika vituo vya afaya wasiwe vikwazo kwa wateja wa mfuko wa bima
ya afya wanapofika kutibiwa kwani wengine wanadai vituo havina dawa ama huduma
sio nzuri wakati wamelipia michango yao kila wakati na hivyo kuwafanya watu
wengine kushindwa kujiunga na mifuko hiyo ya jamii
Aliongeza
kuwa dunia ya sasa lazima kila mtu kuwa na bima,hivyo viongozi na wahudumu wa
afya lazima kuanzisha program maalumu ya kutoa elimu ndani ya jamii ili kila
mtu apate kuelewa na kujua faidia za kujiunga na mifuko hiyo
Pia Bendera
alitoa onyo kwa wateja wa mifuko hiyo ya jamii wanaotumia kadi kwa matumizi
tofuauti na wale amabo wanawaingiza wategemezi wasiotakiwa katika mfuko kwa
maslahi yao binafsi kuacha tabia hiyo kwani wanadidimiza maendeleo katika jamii
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka mfuko wa Bima ya Afya Dkt.Raphael
Mwamoto,alisema kuwa lengo la mkutano huo wadau ambao hufanyika kila mwaka ni
kuangalia changamoto zinaukabiliamfuko na wadau kwa ujumla ambao ni wateja wa
mifuko hiyo
Mwamoto
alisema kuwa Mfuko wa Bima ya Afya umesajili maduka ya dawa muhimu 35 katika
mkoa wa morogoro na wanampango wa kusajili duka moja kwa kila kata kama
wajasiriamali watakuwa mstari wa mbele katika Kujenga maduka hayo ikiwa ni njia
ya kupeleka huduma karibu zaidi na wanachi
Alisema kuwa
wanampango wa kutoa zawadi kwa kila kiongozi wa siasa atakayekuwa mstari wa
mbele katika kutoa elimu ya bima ya afya katika eneo lake,ikiwa kama ni motisha
katika utendaji wa viongozi katika kutekeleza jukumua kwa nia ya kuboresha
zaidi huduma ya afya kwa jamii
Naye Meya wa
Manispaa ya Morogoro,Amir Nondo alisema kuwa wao kama viongozi wa siasa
wameshajipanga kuhakikisha zoezi la kuelimisha jamii kuhusu mifuko ya jamii na
wataanza kwa viongozi kwanza na jamii nzima ya mkoa wa morogoro ili kuweza
kuapata huduma hii
Nondo
alisema kuwa suala la afya ni muhimu kwa kila mwanajamii hivyo kila mtu
anapaswa kujiunga na mifuko hiyo ya jamii kwani itawasaidia kwa kiasi kikubwa
wanapaotwa na matatizo ya kutibiwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment