Eneo la barabara ya kichangani lililoharibiwa na mvua na kusababisha wananchi kukosa mawasiliano. |
Kaimu Mhandisi Manispaa ya Morogoro,Ndelembi Sangija akitoa maelekezo kwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Aziz Abood kuhusu ujenzi wa barabara ya Kitope |
Mbunge wa Jimbo la Morogoro,Aziz Abood akiteta jambo na Mhandisi Ndelembi.
Mbunge,Aziz Abood akiwasalimia wafanyabiashara katika eneo la shule ya msingi Bungo.
Mbunge wa Morogoro mjini,Aziz Abood kulia akikagua barabara ya kitope. |
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro,Aziz Abood ametoa kiasi cha milioni tatu kwa ajili ya ujenzi wa kivuko cha Nakutu na Chalumbi katika kata ya Kilakala vilivyoharibiwa na mvua na kusababisha wakazi wa kata hiyo kukosa mawasiliano na kushindwa kupata huduma mbalimbali za kijamii
Akiwa katika
ziara ya kukagua miundo mbinu ya barabara ndani ya manispaa morogoro,Abood
alisema kuwa barabara nyingi ziko katika hali isiyoridhisha japokuwa nyingi
ujenzi unaendelea na hivyo kuiomba halmshauri hiyo kuendelea kutia nguvu na
kuhakikisha wanchi wanapata barabara safi na zinapitika muda wote
Alisema kuwa
vivuko hivyo vya Kata ya Kilakala vimearibika kwa muda mrefu na hakuna jitihada
zimeanza kuonyeshwa katika ukarbati wake,hivyo ametoa kiasi cha shilingi
milioni 3 zianze ujenzi huo na kwa kushirkiana na halmashauri wakahakikisha
wanachi wa eneo hilo wanapata huduma hiyo ya barabara
Abood
alisema halmshauri inatengeneza barabara kwa kiwango cha lami zenye ukumbwa wa
kilomita 3.3 na kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.148,fedha hizo zimetoka mfuko
wa barabara na kuiomba halmashauri kuendelea na usimamizi mzuri wa fedha hizo
ili wananchi waone maendeleo yanayoletwa na serikali ya chama cha mapinduzi
Aliongeza
kuwa kuna barabara zimetengenezwa ndani ya mwaka mmoja lakini zimeshaharibika
tayari,zina mashimo,ikiwemo barabara ya kuelekea daraja la mwere hivyo kumtaka
mkandarasi aliyetehusika kufanya marekebisho hayo kwani inaonyesha jinsi gani
barabara hazitengenezwi kwa ubora unaotakiwa
Pia alisema
katika eneo la kichangani walipopatwa na mafuriko na wanachi kukosa barabara
watakaa na halmashauri na kuona jinsi gani ya kufanya ili kukarabati barabara
hiyo ili kuweza kurudisha mawasiliano kwa wakazi hao ambao hivi sasa wanatumia
daraja dogo walilotengeneza wenyewe ambalo halina ubora wowote na linaweza
kuleta mahafa muda wowote.
Kwa upande
wake Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Morogoro Ndelembi Sangija alisema kuwa
barabara zote zizoliharibiwa na mvua za mwezi wa nne zina mashimo manispaa iko
katika mkakati wa kuzikarabati na kuhakikisha zinarudi katika hali ya awali.
Sangija
alisema kuwa barabara ambazo zinajengwa kiwango cha lami ziko chini ya kampuni
ya CGT-Contractor Ltd,na mhandisi Stephen Aloyce,hivyo wanachi watakiwa kumpa
ushirikiano wa kutosha kule ambako anafanya kazi ya ujenzi huo ili kuweka
manispaa hiyo katika hali ya kuvutia na yenye maendeleo kwani ubora wa barabara
na nzuri zinavutia pia wawekezaji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment