Tuesday, June 10, 2014

MREMBO WA MKOA WA MOROGORO KUPATIKANA JUNE 13,KATIKA HOTELI YA NASHERA.



Warembo wakiwa katika picha za mapozi.


Pozi la warembo.

Warembo wakiwa katika picha za pozi katika hoteli ya savoy wanakofanyia maandalizi ya mashindano.
JUMLA ya warembo 13 wamejitokeza kuwania taji la kumsaka Miss Morgoro katika shindano litakalofanyika june 13,katika hotel ya Nashera  ambaye atakayewakilisha mkoa katika shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania  kwa mwaka 2014.


 Mwandaji wa mashindano hayo kutoka Kampuni ya FG art Promotion and Internatainment  Asha Saleh aliema kuwa kwa mwaka huu wamejipanga vizuri kuhakikisha mrembo atayewakilisha mkoa wa morogoro atakuwa mrembo wa taifa na kufanya vizuri mashindano mengine.

 Alisema kuwa  majina ya warembo hao ni Lucy Julius,Alexia Shayo,Mwajuma Ibrahimu,Angel Shiyo,Sia Mtui,Bossa Emanuel,Neema Nachenga,Prisca Mengi,Welu Eliud,Hawa Mshana,Lisa Adam Mdolo,Magreth David na Careen Experies 

 Saleh  alisema  kuwa kambi ya warembo hao iko chini ya mwalimu mzoefu sana katika suala la urembo,Salvina Kibona ambaye ni mtaalamu wa  kutosha na anaamini warembo hao watakuwa ndani ya uangalizi mzuri na nidhamu ya hali ya juu kwani nidhamu ndio kipao mbele za kupata mtrembo mwenye vigezo

 Alisema kuwa shindano hilo kwa mwaka huu litafanyika katika hoteli ya nyota tano,Nashera hotel,na kuomba wadau wa urembo kujitokeza kwa wingi kuona mrembo atayewakilisha mkoa wa morogoro katika taifa kutokana na mwaka huu kuwa na ushindani mkubwa sana kuliko miaka iliyopita.

 Naye mwalimu wa warembo hao Salvina Kibona alisema kuwa warembo hao wako katika uangalizi wa kutosha na wanafundishwa mambo mbalimbali ya urembo na jamii kwa ujumla kwani wakishamaliza sula la urembo wanarudi katika jamii na hivyo kuweza kutumia elimu hiyo katika kuendeleza na maisha yao.

 Kibona alisema kuna baadhi hya jamii inakuwa na mtazamo taofuati kuhusu sula na urembo na kusema ni uhuni,jambo hilo sio kweli na kuwatoa watanzania wasiwasi kwa hilo kwani urembo nia ajira kama nyingine kwani wapo watu wengi sana wamefaidika kupitia sekta ya urembo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment