Mariam Said na Mumewe Mtonga wakiwa ndani ya mahakama ya hakimu mfawidhi wa mkoa wa morogoro wakisubiri kusomewa shitaka. |
Mariam Said akiwa nje ya mahakama,anashitakiwa kwa kosa la kumtunza mtoto Nasra ndani ya box miaka minne. |
Baba Mzazi wa Nasra,Rashidi Mvungi(kushoto) akiwa mahakamani na Mariam Said na mumewe Mtonga wakiwa mahakamani. |
UMATI wa watu umekusanyika katika
mahakama ya hakimu mkazi Mkoa wa Morogoro kusiliza kesi iliyokuwa inawakabilia
Rashidi Mvungi baba wa Nasra ,Mariam Said na Mtonga Omari kwa kosa la kumtesa
mtoto Nasra Rashid kwenye box kwa miaka mine na hatimaye kufariki 1/06
Akisoma shitaka hilo Wakili
mwandamizi wa serikali Sunday Hyera,mbele ya hakimu mfawidhi mahakama mkoa Mary
Moyo,alisema kuwa watuhumiwa awali walishtakiwa kwa makosa mawili,la kwanza
kula njama na pili la ukatilia kwa mtoto Nasra
Wakili wa serikali mwandamizi
Sunday Hyera mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa morogoro Mary Moyo
kuwa awali kesi hiyo leo ilipangwa kuanza kusikilizwa lakini
kutokana na mwaathiriwa mtoto Nasra Mvungi kufariki dunia juni mosi
mwaka huu hivyo washtakiwa wote wanapaswa kuhojiwa upya na polisi.
Wakili wa serikali Hyera
aliyekuwa akishirikiana na wakili mwenzake wa serikali Edgar Bandulaki na
mwandesha mashitaka wa polisi Inspekta Zabron Msusi wameiombia
mahakama kuwa baada ya washtakiwa wa kesi ya awali kuhojiwa na polisi kesi hiyo
itapangwa haraka mahakamani kwa ajili ya kutajwa.
Kwa upande wake Hakimu mkazi
mfawidhi wa mkoa wa Morogoro Mary Moyo alikubaliana na ombi hilo la
wakili wa serikali na kupanga kesi hiyo hiyo kutaja tena juni kumi na mbili
mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilionekana kuvuta
hisia za watu wengi wakazi wa manispaa ya morogoro na nje kufurika viwanja vya
mahakama huku wengine wakishindwa kujizuia na kuangua kilio mahakamani hapo na
wengine kuwazomea watuhumiwa wakati wakipandishwa kwenye gari chini ya ulinzi
mkali wa polisi wakiepelekea kituo kikuu cha polisi kati mkoa
wa Morogoro kwa mahojiano upya.
Mwisho
No comments:
Post a Comment