Friday, June 6, 2014

MHANDISI WA HALMASHAURI YA MOROGORO SULEMAN KATOTO APATA AJALI NA KUFARIKI DUNIA.


Gari alilokuwa anatumia marehemu Suleman Katoto na kupata ajali katika eneo la kihonda mjini Morogoro


Mhandisi Suleman Katoto akiwa na Mwenyekiti wa Halamshauri ya Morogoro Kibena Kingu enzi za uhai wake.

Gari alilopata nalo ajali na kufariki dunia papo hapo Mhandisi Suleman Katoto.

                                                                
                                                                
Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Selemani Katoto (41) amefariki dunia papo hapa baada ya gari alilokuwa akiendesha kugangana uso kwa uso na gari jingine eneo la Kihonda Maghorofani.

 Kaimu kamanda wa Polisi mkoani Morogoro John Laswai alisema ajali hiyo ilitokea Juni 4 mwaka huu majira ya saa 5:30 usiku barabara ya Kihonda-Modeko baada ya gari aina ya Toyota Cresta saloon yenye namba za usajili T 908 iliyokuwa ikiendeshwa na mhandisi Katoto

 Kamanda alisema gari ya  marehemu iligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T403ABF iliyokuwa ikiendeshwa na Gabriel Temba(41) na kufarikia papo hapo

 Alisema kuwa mhandisi Katoto alikuwa akitokea maeneo ya Ipoipo Modeco kuelekea kihonda maghorofani na ndipo alipogongana na gari hiyo iliyokuwa ikitokea kihonda kuelekea ipoipo na kusababisha kifo cha mhandisi huyo.

 Kamanda huyo alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa mhandisi huyo ambaye alifariki dunia papo hapo baada kutokea kwa ajali hiyo.

Mwili wa mhandisi huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro na polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi.

 Kwa mujibu wa familia ya marehemu mhandisi huyo atazikwa kijiji cha mkono wa mara Wilaya ya Morogoro. 

Mwisho..

No comments:

Post a Comment