Wednesday, June 4, 2014

MAMIA WAJITOKEZA KUMUUAGA MTOTO NASRA.

                                                    
Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa mtoto Nasra tayari kupelekwa katika makaburi ya Kola kwa mazishi.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza na wananchi waliojitokeza katika zoezi la kuuaga mtoto Nasra Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Mwili wa Mtoto Nasra Rashidi ukiwa ndani ya gari katika uwanja wa jamhuri morogoro na kupelekwa makaburi ya kola

Mjumbe wa Bakwata Mkoa wa Morogoro,Ally Omar akitoa neno katika mazishi hayo.
WANANCHI wa Manispaa ya wamesimamisha shughuli zao kwa takribani saa tatu kushuhuduia tukio la kumuaga mtoto Nasra Rashid Mvungi aliyefariki tarehe 1/06 baada ya kuuguzwa kwa muda mrefu kutokana magonjwa aliyoyapata baada ya kutunza  ndani ya box kwa miaka 4 bila kupata huduma muhimu

Wananchi hao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Joel Bendera,mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Azizi Abood,na viongozi wa dini mbalimbali,taasisi za kutetea haki za binadamu,walijawa na huzuni kubwa kwa kitendo kilichofanywa na mama huyo cha kumtesa mtoto Nasra

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza kwa uchungu alisema kuwa kitendo kilichofanywa na familia hiyo ni cha aibu sana katika jamii  hakiwezi vumiliwa kamwe na hakuna dini yoyote inayokubali kitendo hicho cha kinyama kilichofanyika

Bendera alisema kuwa mateso aliyopata mtoto Nasra ni makubwa sana na yakusikitisha sana na walitenda kitendo hicho watateka sana na malipo yao yatakuwa hapa hapa duniani kutokana na kwamba wazazi hao walikuwa wanaamka asubuhi wanaenda kwenye biashara zao na kumwacha malaika wa mungu anateseka ndani kwa miaka 4

Alisema kuwa binadamu tumeumbwa tuwapende watoto tuonawaza lakini kwa wazazi hawa ilikuwa tafuoti kabisa na kufanya unyama wa kutisha kwa mtoto nasra rashidi kwani hao ndio wamesababisha kifo chake na mwenye mungua atawalipa hapa hapa duniani

Alimtaka hakimua anayesimamia kesi hiyo kuhakikisha watuhumiwa hao hawataachiwa na kupata mateso zaidi waliyomfanyia mtoto Nasra Rashi kwa kipindi cha maika mine bila aibu yoyote na kumsababishia mauti

Bendera alisema kuwa yeye kwa kushirikiana na serikali watahakikisha kuanzia baba wa mtoto (Rashidi Mvungi) na watuhumiwa wengine hawataachiwa hata kwa njia za panya wakitoka watarudshwa tu rumande ili iwe fundisho kwa jamii nyingine yenye tabia kama hiyo

Pia aliwataka vingozi wa serikali za mitaa na familia kwa ujumla kuwa na tamadauni za kutemeleana na kujualiana hali ili kuweza kugundua ndugu wanaishi katika mazingira gani kutokana na majirani wangekuwa karibu na Mariam Said wangegundua mtoto huyo mapema

Aidha aliwaonya wazazi wanaopata watoto nje ya ndoa na kuwatelekeza kuacha tabia hiyo,na kusema kuwa Mvungi atalaaniwa kwa kitendo alichofanya cha kutokujua hali ya mwanae mpaka mauti inamkuta na kungangania maiti akazike yeye.

“Ndugu yangu Mvungi,sina woga na siogopi chochote,kitendo ulichofanya cha kumtelekeza binti  Nasra ni  cha kinyama na hakikubaliki na jamii yoyote na hivyo utalaaniwa milele ile duniani”Alisema Bendera

Azizi Abood anena.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro,Azizi Abood alisema kuwa kitendo hicho kimekuwa sikitiko nchi nzima na aibu kubwa kwa watu wa morogoro kwani haijawahi tokea binadamu anamtesa mtoto na kumlea kama mnyama ndani ya nyumba

Abood alisema kuwa anaungana na mkuu wa mkoa Joel Bendera katika kuhakikisha watuhumiwa hawataachiwa na watapatiwa adhabu kali ambayo itakuwa funzo kwa jamii ya Tanzania

Alisema kuwa kama kuna tetesi zozote zinaonekana kuna watu wengine wanafanya unyama kama huo taarifa ilitolewe ofisini kwake na yeye yuko tayari kulea watoto wote wanatelekezwa na wazazi wao
Ujumbe wa Bakwata.
Naye Mjumbe  wa Bakwata Mkoa wa Morogoro,Ally Omar alisema kuwa kwa dini ya kiislamu watu hao wamefanya kinyume na maadil ya dini,kwani dini inafundisha upendo na amani katika familia ila ndugu zetu hawa hawakuwa na upendo kwa mtoto Nasra kabisa

Shehe Omar alisema kuwa kwa mazingira aliyokuwa anaishi mtoto Nasra yanasharikishwa na imani za kishirikina ndani yake,alimfanya mtoto msukule katika biashara zao wanafanya kila siku

Alisema kuwa watuhumiwa hao watapata adhabu kali duniani na mbinguni na mtoto Nasra anaenda peponi daima kutoka na kusababishiwa kifo,kwa kupata mateso makali kwa kipindi cha miaka 4 bila kupata huduma muhimu za kijamii

Mjumbe huyo aliitaka serikali pia kuangalia upande wa majirani wa watuhumiwa,kwa kipindi hicho chote hawakuwa kumuona mtoto huyo,hata kumsikia kama kuna mtoto ndani ya nyumaba hivyo inabidi majirani nao wahusike katika hilo

Wananchi Wanena.
Bwende Waziri alisema kuwa jamii ya sasa imekuwa haina huruma kabisa kwa watoto wanaowazaa wenyewe,kitendo kilichotokea ni aibu kwa wazazi hao na hawakuwa na malengo mazuri na mtoto huyo asiyekuwa na makosa yoyote hapa duniani

Waziri alisema kinachotakiwa kufanyika hivi sasa ni serikali kuipitia hata kwa viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele katika kukemea vitendo vyote vya ukatili vinavyotendeka katika jamii kutokana na binadamu kutokuwa na upendo na imani na watoto wao.

Polisi.
Baaada ya zoezi la kuuaga mwili wa Nasr Rashidi katika uwanja wa jamhuri mjini Morogoro askari kanzu walimchukua Mzee Mvungi na kumpakia katika gari na kumrudisha rumande na wala hakupata nafasi ya kwenda makaburini kumzika mwanae.

No comments:

Post a Comment