Monday, July 8, 2013

WAMTAKA WAZIRI WA ARDHI KUINGILIA MGOGORO WA ARDHI.


WAKAZI  wa kijiji cha Lubumo,kata ya Kidugalo wilaya ya Morogoro
 wamemuomba waziri wa ardhi nyumba na makazi kuingilia kati mgogoro  wa
ardhi kati yao na jamii ya wafugaji wa kimasai kutokana na maeneo makubwa waliyokuwa wakitumia kwa kilimo kupewa wafugaji  .

Afisa mtendaji kijiji cha Lubumo Khasan Ngalen,Mwenyekiti wa kijiji cha Lubumo Juma Rajab Mgodom na katibu wa CCM tawi la Lubumo Yahaya Husein walisema kuwa  inaonekata  serikali ya wilaya imeshindwa kutatua mgogoro huo na kusababisha mapigano ambayo yanaweza kutokea muda wowote na kusabanbisha hasara kubwa katika jamiii.


Walisema kuwa waliohusika kuuza maeneo yao ni kijiji cha jirani cha Selegeti B kwa  kushirikiana na  viongozi wa kata ya Kidugalo  bila kushirikisha wananchi ambao ndiyo wamiliki wa mashamba na bila kufuata taratibu za kuuza mashamba kwa kutumi vikao halali vya vijiji.

Walisema kuwa wakazi wa kijiji hicho hawana maeneo ya kulima kutoka na na maeneo mengi kupewa wafugaji na hivyo kutasababisha wakulima kuvamia maeneo hayo kwa ajili ya kilimo na kunaweza kutokea kutokuelewana kama seriklia haitachukua hatua stahiki mapema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro Julias Madiga alisema kuwa  taarifa ya mgogoro huo haijafika ofisini kwake  hivyo anashangaa kuona wananchi  hawashirikishi  viongozi katika kutatua matatizo
yao.

Hivyo aliwaomba viongozi wa kijiji wakishirikiana na viongozi wa kata kutoa
taarifa hiyo kwenye ofisi yake ili waweze kutatua kero hiyo nakutafutia ufumbuzi
haraka ili kuzuia vurugu ambazo zinaweza kutokea na kusababisha madhara makubwa katika jamii zote mbili.

No comments:

Post a Comment