Friday, October 13, 2017

AMRI YA MKUU WA WILAYA YASHINDWA KUTEKELEZWA.

Augusti 28 mwaka huu katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Morogoro, Regina Chonjo aliagiza kuondolewa mara moja kwa vituo vyote vya kuoshea magari vilivyojengwa katika maeneo yasiyo rasmi, na kuwataka maafisa wa Mipango miji kuacha kutoa vibali kiholela vya ujenzi wa vituo hivyo,kwani maeneo hayo yametengwa kwa matumizi maalumu. 

Hata hivyo agizo hilo limeonekana  kupuuzwa, kwani baadhi ya vituo vinavyomilikiwa na viongozi ndani ya baraza hilo, vinaonekana kuendelea kufanya kazi, huku vikiwa vimejengwa katika maeneo yasiyo rasmi.

 Mkazi wa Manispaa ya Morogoro,Constatino Diego alisema kuwa agizo la mkuu wa wilaya linashindwa kutekelezwa kutokana na vituohivyo kumilikiwa na baadhi ya vigogo ndani ya manispaa hiyo ambao ndio watunzi wa sheria ndogo.

“tunaomba serikali ya mkoa kuingilia kati sakati hili ili haki itendeke kwa watu wote,sheria haichagui haingalii cheo cha mtu,wahusika wachukuliwe hatua za kisheria na kuondoka katika maeneo hayo ya wazi”Alisema 

John Mgalula ni Mkurungezi wa Manispaa ya Morogoro, yeye anakiri kuchelewa kuchukuliwa hatua kwa utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, huku  akibainisha hatua zinazoenda kuchukuliwa katika kutekeleza agizo hilo.

 Mgalula alisema Sheria ndogo na miongozo inayosimamia Manisapaaya Morogoro inatoka ndani ya Baraza hili, lakini baadhi yao wamekuwa ndiyo wa kwanza kukiuka sheria wanazozitunga, huku Kiongozi wa Madiwani katika Halamshauri hii, akiwa wa kwanza kuwataka kufuata miongozo hizo.

 Manispaa ya Morogoro iko katika mchakato wa kuelekea kuwa Jiji, lakini kutokana na changamoto mbambali zimeendelea kuchelewesha mchakato huko.   huku mpangilio usioridhisha wa baadhi ya miundomoni, ikonekana  kuchangaia.
 Mwisho.

No comments:

Post a Comment