Na,Peter Kimath.
WANANCHI wa Kijiji cha Mfumbwe Tarafa ya Mkuyuni Wilaya ya Morogoro wamesema mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuundwa kwa mabaraza ya ardhi kumesaidia kupunguza migogoro ya ardhi iliyokuwainatokea na kuleta madhara ndani ya jamii.
Kabla ya zoezi la mpango wa
matumizi bora ya ardhi,baraza lilikuwa linapokea migogoro kumi na tano kwa
mwezi,lakini hivi sasa wanapokea kesi mbili tu,ambazo huzitolea suluhu na
kuishia ndani ya baraza.
Hayo
yalitolewa na Mwenyeiti wa baraza la ardhi, Siad Kisukari katika mdahalo
ulioandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Uluguru Mountains
Agricultural Development Project (UMADEP) kupitia PELUM Tanzania,uliokuwa
unajadili faida za mabaraza ya ardhi na mpango wa matumizi bora ya ardhi
kijijini hapo.
Kisukari
alisema baraza linafanya kazi kwa mujibu wa sheria,na hiii inatokana na baada
ya wajumbe kupata elimu,na wananchi kuelimishwa umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria,pamoja
na kuwa hati miliki zinazotambulika.
Paulina
Daniel alisema migogoro iliyoko katika kijiji hicho ni mashamba ya urithi ambayo
hugombaniwa na familia,maeneo ya taasisi kuvamiwa na wananchi,na upanuzi wa
barabara unaopelekea mashamba mengi kumegwa.
Ramadhani
Fufumbe alisema kuwa ukosefu wa elimu katika famiia ndio unachangia kuleta
migogoro ya kugawa mali za marehemu,ndio maana migogoro ya miradhi ipo sana
kijijini hapo.
Kwa
upande wake,Afisa Miradi kutoka UMADEP,Pessa Kusaga aliwataka wananchi
kuhakikisha ardhi wanaoyoitumia inamilikiwa kisheria ili kuepuka migogoro ya
mara kwa mara ambayo huleta uvunjivu wa amani.
Kusaga
alisema kuwa faida za kuwa na hati miliki,unaweza kupata mikopokatika taasisi
za kifedha,kupunguza migogoro,na pia eneo likiwa katika mpango wa matumizi bora
ya ardhi unakuwa na uhakika na eneo lako.
Afisa
Mifugo kutoka halmshauri ya morogoro,Pius Ntanga aliwataka wafugaji kuacha
zoezi la kuhamisha mifugo,kupunguza mifugo ili kufuga kisasa kwa lengo la
kuepuka migogoro kati yao na wakulima.
“kila
mwananchi azingatie eneo kwa magumizi husika yaliyopangwa,mfugaji baki kwenye
eneo la malisho,mkulima baki kwenye eneo la kulima,atayemwingilia mwenzake
hatua kali zitachukuliwa dhidi yake”Alisema.
Mwiho.
No comments:
Post a Comment