SERIKALI
mkoani Morogoro imetoa wiki mbili kwa uongozi wa halmashauri ya
Malinyi,kuchukua uamuzi wa kuwapokonya mashamba wananchi ambao wamekumbatia
mashamba katika skimu ya Umwagiliaji ya Alabama bila kuyaendeleza.
Mashamba hayo
yatolewa upya kwa wananci wenye uhitaji wa kuendeleza kilimo katika Skimu
hiyo,kwani hakuna haja ya kukumbatia ardhi wakati kuna wengine wanahitaji
kuendeleza kilimo.
Mkuu wa Morogoro
Dr Kebwe Stephen, alisema haiwezekani serikali imepoteza zaidi ya bilioni 6 kwa
ajili ya kuwajengea Skimu hiyo, lakini jambo la ajabu kuna baadhi ya wananchi
wamekaa na mashamba bila kuyaendeleza, wakati wapo vijana ambao wanataka
kujihusisha na kilimo katika mashamba hayo hata kwa kukodishiwa.
Alisema
serikali ilitoa kiasi cha shilingi billion 6 kwa ajili ya ujenzi wa skimu hii
ya umwagiliaji, mradi ambao unafursa pekee kwa wakazi wa Itete na wilaya
Malinyi, kufanya kilimo cha mazao mbalimbali msimu mzima wa mwaka.
Mkazi wa
Itete,Salum Mkola aliiomba serikali kuwawezesha katika kukabiliana na
changamoto zinazowakabili, hususani katika upande wa elimu, juu ya kilimo
cha umwagiliaji,kwani kuna baadhi wameshaanza kufaidika na kilimo hicho,huku
wengine wakikosa ujuzi wa kilimo cha kisasa.
Makamu
Mwenyekiti Halmshauri ya Malingi,Severus Kamguna alisema kero za wakulma
zinashughulikiwa pamoja na kuwaondoa
wale wote wanaoendelea kukumbatia mashamba hayo bila kuyaendeleza.
Skimu ya
umwagiliaji ya Alabama ina jumla ya hekta 8000 lakini mpaka sasa ni ekari
1800 ambazo zinazotumika kwa kilimo na shughuli za kilimo hufanyika
kipindi chote cha mwaka.
Mwisho..
No comments:
Post a Comment