WANANCHI wa Kijiji cha Mela kata ya
Melela Wilayani Mvomero wamesema ili kupunguza migogoro ya ardhi,kila kijiji
kipimwe na kuanishwa mipaka,kila mwananchi apimiwe eneo lake analoishi kwa
lengo la kuepuka mwingiliano.
Hayo yalibainishwa katika mdahalo
uliofanyika katika kijiji cha Mela,uliokuwa unajadili nini kifanyike ili
kupunguza migogoro ya ardhi,uliondaliwa na Shirika la Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yanayofanya kazi na wakulima na
wafugaji wadogoTanzania (PELUM)
Kishakwi Mlimba alisema
kuwa migogoro mingi inasababishwa na wananchi kutokujua mipaka ya eneo
analomiliki,hivyo kama watapimiwa maeneo yao wanayomikili na kupewa hati miliki
kwa kila mmoja itapunguza mwingiliano na kila mtu kujua mipaka yake.
“naomba serikali na wadau
kutusadidia kupima kijiji chetu,kiwe kwenye matumizi bora ardhi,hatupendi
migogoro ya ardhi itokee kwani inaurudisha nyuma katika shughuli za maendeleo.”Alisema.
Naye Sayota Singa alisema
kinachofanya jamii ya wafugaji kuhama hama ni ukosefu wa maji kwa mifugo,na matumizi
ya binadamu,hivyo ili kuzuia wafugaji kukaa sehemu moja lazima serikali iweke
miundo mbinu mizuri ikiwa ni pamoja na maji ya kudumu kuwepo.
Singa alisema kuwa katika kijiji cha
Mela kuna mashamba pori,yapo kwa muda mrefu bila shughuli yoyote,hivyo aliiomba
serikali kabla ya kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi mashamba hayo
yatambuliwe,ardhi ipo ila idaid ya wananchi inaongezeka kila siku, hivyo ardhi
kama haitumiki ipewe wananchi waiendeleze kulikoa kuwa pori
Kwa upande wake,Afisa
Miradi,kutoka PELUM,Rehema Fidelis alisema kuwa lengo la wananchi kuwa na
mipango ya ardhi ni kuhamasisha kilimo endelevu ndani ya jamii,wananchi kuwa na
ushiriki katika kusimamia sekta ya kilimo.
Fidelis alisema
mpango wa matumizi bora ya ardhi utafanyika katika vijiji 30,kwa kushirikiana
na halmashauri husika,wananchi watapimiwa ardhi yao na kuingizwa kwenye
matumizi yanayotambulika ili kupunguza migogoroya ardhi.
No comments:
Post a Comment