Monday, October 31, 2016

WANANCHI WA VIJIJI VYA KIBAONI,MELELA,MAGALI,WILAYANI MVOMERO WAJADILI MIGOGORO YA ARDHI.

                                              
Afisa kutoka shirika la UMADEP,Pesa Kusaga,akitoa ufafunuzi kwa wananchi wa kijiji cha Kibaoni juu ya maswala ya Ardhi
Mfugaji wa Kijiji cha Kibaoni,Mvomero,Joshua Saning'o akichangia mada kwenye mdahalo wa nini kifanyike kupunguza migogoro ya ardhi.
Mhadhiri wa chuo cha SUA,Mr.Malisa akizungumza na wananchi wa Kibaoni jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi ndani ya jamii.
Mkulima,Catherine Iddy,akichangia mada katika mdahalo wa nini kifanyike katika kutatua migogoro ya ardhi,ulioandaliwa na PELUM  na kutekelezwa na shirika la UMADEP.

MIGOGORO ya Ardhi katika kata ya Melela Wilaya Mvomero inasababishwa na viongozi wa serikali ya vijiji,mabaraza ya ardhi ya vijiji kutoitisha vikao,kutumia madaraka vibaya,kupokea rushwa na kupelekea kuwa chanzo cha machafu na uvunjifu wa amani ndani ya jamii.

Hakuna vikao vinavyoitishwa ndani ya vijiji vya kufanya maamuzi sahihi miradi ya maendeleo vinavyofanyika ndani ya kijiji,viongozi wanajichukua maamuzi wenyewe na kuandika muhtasari hewa ya kikoa,hivyo kupoteza uaminifu kwa wananchi wanaowaongoza.

Hayo yamebainishwa katika midahalo wa nini kifanyike kutatua migogoro ya Ardhi,ulioandaliwa na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi na wakulima wadogo Tanznia.(PELUM),katika mradi wa Ushiriki wa wananchi katika kusimamia sekta ya Ardhi(CEGO),uliofanwa na UMADEP katika kijiji cha  Kibaoni,Melela na Magali,wilaya ya Mvomero.

Mkulima wa Kibaoni, Catherine Iddy alisema viongozi wanafanya kazi kwa mazoea,pindi inapotokea mgogoro wa mkulima na mfugaji,viongozi wanakuwa upande wa mfugaji kutokana na kujua wanapata fedha kwake,na kuwafanya wakulima kuwa wanyonge na kutojua pakupeleka malalamiko yao.

Catherine alisema ili kumaliza migogoro ya ardhi,lazima vijiji vipimwe ili kutambua mipaka,na wakulima na wafugaji kutengewa meneo yao,na kila mwananchi kuheshimu mipaka ya mwenzie bila kuingiliana.

Mfugaji Joshua Saning’o alisema kuwa migogoro ya wakulima na wafugaji itamalizika tu pale serikali itapoweka miundo mbinu ya maji kwa ajili ya mifugo,hii itawafanya wafugaji kutohama hama kwa lengo la kutafuta maji na kubaki katika eneo walililotengewa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Magali,Steven Msimbe alisema kuwa wafugaji wamekuwa kero katika hicho,wanalisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima na kula mazao,wanapeleka mifugo kunywa maji kwenye vyanzo vya maji,na kuchafua maji yanayotumiwa na wananchi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Wasaidizi wa Kisheria,Flora Masoy aliwataka viongozi na wananchi kushirikia katika vikoa vya maamuzi vinavyofanyika,pia kutumia sheria zilizowekwa katika kutatua migogoro ya ardhi sio kutumia suluhu ya wenyewe,ili kupunguza migogoro ya ardhi.


No comments:

Post a Comment