Saturday, October 22, 2016

MSANII BAZGAR AIBUKA NA KIBAO KIPYA,"NIPO"

                                  
 MSANII wa Bongo flavour,Salum Nyamunga(Bazgar) mwenye maskani yake Dumila Wilayani Kilosa amekuja na wimbo wake mpya unaojulikana kwa jina Nipo,alioutengenezea katika studio za Dizz Power.

Nyamunga alisema wimbo Nipo,anawaambia mashabiki wake bado yupo kwenye game ya bongo Flovour baadaya kupotelea kwenye siasa kwa muda mrefu,na kuwajulisha bado anafanya siasa na muziki kwa pamoja

“mashabiki wangu nipo,nimerudi kwenye game, karibuni sana kuniunga mkono,na mimi sintowaangusha katika kazi zangu za muziki”Alisema Bazgar.

Alisema kuwa wimbo wa Nipo,ni wimbo wa tano katika nyimbo zake aliwatoa,zilizotengenezewa katika studio za Dizz Power na Bamiza zote kutoka mjini Morogoro.

Bazgar ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Dumila,alisema kuwa katika muziki msanii anayemkubali ni Afande Sele na AY,hii ni kutokana na utunzi wao wa mistari yenye kuelimisha jamii na kukubalika kwao ndani na nje ya Tanzania.

Pia aliwataka wasanii waliopo kwenye tasnia ya muziki wakumbuke kuwa muziki ni biashara, hivyo wanatakiwa kujiamini,kujituma  kutengeneza kazi zinazokubalika ndani ya jamii na zenye kuelimisha.


No comments:

Post a Comment