UMOJA wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi,Wilaya ya Morogoro mjini,umeiomba serikali kukaribisha wawekeza wengi
kuwekeza ndani ya mkoa kutokana na kuwa na meneo ya wazi ya kutosha,na nguvu
kazi za vijana kufanya kazi katika viwanda vitakavyojengwa.
Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa
umoja huo,Salum Mkolwe wakati wakiadhimisha kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha
baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere,ambapo waliadhimisha kwa kufanya usafi katika
eneo lao lilipo Tungi,pamoja na kufanya tamasha la michezo.
Mkolwe alisema katika mkoa wa morogoro
kuna mashamba pori mengi,hivyo ni wakati wa serikali kukaribisha wawekezaji
kuja kujenga viwanda,ambavyo vitainua uchumi wa mkoa,pamoja na vijana kupata
ajira za kudumu na kuepuka utegemezi
Alisema katika kumkumbuka hayati Baba
wa Taifa Mwalimu Nyerere wameamua kumuenzi kwa kufanya usafi katika eneo lao
wanalomiki lilipo tungi ambalo litatumika kama kitenga uchumi chaumoja huo,pia
kufanya michezo mbalimbali ikiwemo mpira miguu,kuvuta kamba na kuimbiza kuku.
“tudumishe usafi wa mazingira,kujenga
afya bora,vijana tuwe mstari wa mbele katika kutunza mazingira,maendeleo
yanapatikana sehemu salama yenye mazingira ya kuvutia.”Alisema.
Pia alisema lazima tudumishe amani
iliyoachwa na Mwalimu,kukiwa na amani na utulivu,kutawakuwa na siasa safi,utawala
bora unaokubalika na maendeleo yatapatikana,hivyo vijana kuwa mstari wa mbele
katika kuitunza amani ya nchi.
Kwa upande wake,Katibu UVCCM,Wilaya ya
Morogoro,Peter Kabwe aliwataka vijana kutumia muda wao kujenga chama na
kukitumika,vijana ndio wenye nguvu,tusiwaachie wazee chama.
Pia alisema kila kijana mwanachama wa
ccm kuwa mbalozi katika eneo analoishi kwa kusema mazuri ya chama,viongozi wa
matawi ya vijana kwa kila kata kuwa mfano ndani ya jamii,pia kuongeza idadi ya
wanachama,kuhakikisha kuna wanachama hai,na wanaolipa ada ili kuimarisha chama
chao.
 |
No comments:
Post a Comment