LICHA ya serikali ya awamu ya tano kutoa fursa ya
elimu,hali imekuwa tofauti kwa watoto zaidi ya 600 Kitongoji cha Namwawala B
wilayani Kilombero, ambapo wamekosa fursa tokana na umbali uliopo toka katika
kitongoji hicho hadi shule ilipo.
Wakizungumza katika mkutano ulioitishwa na Mkuu Wa
wilaya ya Kilombero James Ihunyo,wakazi wa eneo la Mikochini katika kitongoji
cha Namwawala wamesema wapo katika eneo hilo kwa miaka 15 sasa bila Huduma
muhimu za kijamii ikiwemo shule.
Walisema kwa sasa eneo la Mikochini lina watoto 600
wanaojisomea katika kibanda kidogo kwa walimu wa kujitolea huku wengine
wakitembea umbali Wa kilomita 18 kufuata elimu katika kitongoji cha Idandu.
Madalu Basu mkazi Wa Mikochini alisema
wamefuatilia suala hilo kwa muda mrefu bila mafanikio na kufanya watoto wengi
kukosa fursa ya elimu hali inayopelekea kuwafanya watoto hao kuwa kuolewa
mapema ama kuwa wachungaji.
Sambamba na shule pia wananchi
hao walisema eneo hilo halina uduma nyingine za msingi kama maji,zahanati na
barabara na kuwafanya wananchi hao wajione kama wapo katika giza.
Akizungumzia suala la kukosa zahanati,Daniana Rajabu
alisema kuwa hali hiyo inapelekea akinamama wengi wajawazito kujifungulia
njiani na inawapa wakati mgumu kwenda kijijini Namwawala kwani inawabidi kuvuka
mito miwili ili kufikia zahanati.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Namwawala B,Machia
Nyambu alisema kwa sasa wakazi Wa Mikochini wapo 4000 na wanaiomba serikali
kuwasajili ili kupata kijiji kutokana na kuwa na sifa zote na baada ya kupata
kijiji Huduma zote muhimu zitapatikana hasa kutokana na wananchi wa eneo hilo
kuwa na moyo wa kujitolea.
Nyambu alisema kwa kuanzia wananchi hao wamejenga
boma kwa ajili ya kliniki NA pia kujenga darasa la miti huku pia wakichimba
Barbara ya kilomita tano kwa kujitolea NA kusema kuwa serikali ikiwaunga mkono
katika kuwajengea shule wao wapo tayari kuchangia shilingi laki tano kwa kila
mmoja ili kukamilisha.
Mkuu Wa Wilaya ya Kilombero James Ihunyo alisema
kuna haja eneo hilo kuwepo shule ya msingi hasa baada ya kubaini uwepo wa
watoto wengi na atatuma wataalamu wa elimu kufika eneo hilo na kufanya tathmini
ili mwaka 2017 watoto waanze shule.
Kuhusu ombi la kupatiwa kijiji,Ihunyo
alisema kuwa taratibu zinabidi zifuatwe kuanzia ngazi za chini ila amesisitiza
kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni kupatiwa Huduma muhimu ikiwemo maji,zahanati na
shule.
No comments:
Post a Comment