JUMUIA ya tawala za mitaa nchini(ALAT)
mkoa Wa Morogoro imependekeza madiwani kutambuliwa na serikali katika mfumo
rasmi wa ajira kwa kuwekwa kwenye utaratibu ambao utaweza kuwafanya wawe na
maslahi mapana.
Pendekezo hilo limetolewa na wajumbe wa jumuia hiyo mkoa Wa Morogoro wakati wakiwasilisha mapendekezo yao kwenda katika mkutano Mkuu wa Alat Taifa utakaofanyika wiki ijayo.
Walisema kuwa madiwani kutambuliwa katika mfumo rasmi wa ajira kutawafanya wawe wenye tija zaidi na kupunguza migongano ya kimaslahi baina ya madiwani na watendaji na pia mfumo huo utasaidia kuboresha hali zao za maisha yao baada ya Utumishi wao kumalizika.
Pia wajumbe hao wamependekeza yawe yanatolewa mafunzo elekezi kwa madiwani na wakurugenzi sambamba na wakuu wa wilaya na yawe yanagharamiwa na serikali ili kuwajengea uwezo madiwani kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Sambamba NA hayo pia wameomba viongozi Wa juu wawe makini wanapotoa matamko yao ikiwemo wanapoondoa Kodi ama ushuru ambao NI vyanzo muhimu kwa serikali za mitaa NA kutolea mfano kuwa kodi ya Mifugo irudishwe NA wafugaji walipe kodi kama inavyofanywa kwa mazao.
Kuhusu mkoa Wa Morogoro kutambuliwa kuwa ghala la chakula taifa,wajumbe hao wameitaka serikali kuufanya mkoa huo uwe rasmi eneo la Kilimo NA kuomba eneo la Ardhi ya akiba irejeshwe kwa wananchi ili litumike kwa Kilimo.
Aidha wameomba serikali kuu iweze kuchangia gharama za kumalizia uchaguzi pale inapotokea kuwapo kwa nafasi wazi na wakurugenzi wawezeshwe bajeti za uchaguzi ili kuwa na viongozi Wa serikali za mitaa.

No comments:
Post a Comment