MKUU wa mkoa wa Morogoro,Dkt.Steven Kebwe amewataka maafisa
lishe katika halmashauri kutoa elimu ya kutokomeza suala la lishe duni,sio
kukaa maofisi na kuapangiwa kazi nyingine tofauti na mikataba yao ya kazi.
Dkt.Kebwe alisema hayo katika kikao cha kujadili na kuweka
mikakati ya kupunguza lishe duni katika halmashauri za mkoa wa Morogoro,Pwani
na Dar es salaam kilichoandaliwa na Partinership for Nutrition in
Tanzania(PANITA) kanda ya Mashariki.
Alisema kuwa katika halmashauri kuna maafisa lishe,ila wamekaa
tu maofisini badala yakuzunguza mitaani na kutoa elimu jinsi ya kumaliza lishe
duni,wafanye kazi walizopangiwa sio kufanya kazi tofauti na mikataba yao ya
ajira.
Dkt.Kebwe aliwataka maafisa lishe kuhakikisha kila mpango kazi katika
halmashauri suala la lishe linaingizwa na kupewa kipao mbele,afya ni muhimu
sana hivyo mtu haiwezi kuzalisha kama hana afya nzuri.
Kwa upande wake Mratibu wa Lishe Kanda ya Mashariki,Gaudencia
Donati alisema kuwa lengo la kukutana ni kupeana uzoefu na kuweka mikakati ya
kutokomeza lishe duni katika maeneo mbalimbali.
Donati alisema suala la lishe duni lazima lishughulikiwe na kila
mtu,kuhakikisha watoto wanazaliwa na afya nzuri,wakina mama wajawazito wapewe
elimu ya kutosha ili kuweza kujifungua watoto wenye afya nzuri.
Mganga wa Manispaa,Baraka Jonas alisema kuwa lishe duni
inasababishwa na ukosefu wa protein,damu na madini joto,hivyo wadau wa afya
washirikiane kuhakikisha virutubisho vinakuwepo katika vyakula mbalibmali
wanavyotumia.
Jonas alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wakina mama wanapata
elimu wanapokwenda kliniki,na umuhimu wa kunyonyesha watoto wao pindi
wanapojifungua ili kuweza kutokomeza lishe duni.
No comments:
Post a Comment