WAFANYABIASHARA
wa soko la Mawenzi lililopo Manispaa ya Morogoro wamesema uuzaji wa bidhaa
sokoni hapo umeshuka kwa kiwango kikubwa kulingana na misimu iliyopita huku
wakifanya biashara bila kuona faida.
Wakizungumza
na Jambo Leo,kwa wakati tafauti,Donatha Urio alisema kuwa soko limekuwa na watu
wengi ila wanaofanya biashara ni wachache sana kutokana na bidhaa kuwa nyingi
ila wanunuzi wachache kutokana na mzunguko wa hela kuwa mdogo sana.
“nakaa
sokoni hapa toka saa moja asubuhi mpaka saa kumi mbili jioni,Napata shilingi
elfu nane kwenye mauzo,wakati miezi miwili iliyopita nilikuwa apata shilingi
elfu hamsini kwa siku”
Shukuru
Leonad alisema kuwa tatizo kubwa ni mzunguko wa hela kuwa mdogo sana,kiasi
kinachochangia bidhaa kushuka bei kila siku,na wanunuzi wananunua kiwango
kidogo kutokana na fedha aliyonayo mfukoni tofauti na miaka mingine iliyopita.
“fungu
la viazi linauzwa shilingi mia mbili kutoka elfu tatu,nyanya ndoo efu moja
kutoka elfu ishirini,hii haijawahi kutokea katika soko letu na inatufanya
tubadili biashara”Alisema.
Leonad
alisema kuwa kuna baadhi ya wafanyabishara wanashindwa kuagiza mizigo mipya
kutokana ya zamani ipo,na bidhaa nyingine hasa matunda na nyanya zinaoza
kutokana na kulimwa kwa wingi na kukosa sehemu ya kuhifadhi kwa matumizi ya
badae.
Alisema
kuwa wafanyabiashara wengi wanaogopa kuweka fedha zao sokoni kutokana na
hawapati faida yoyote,ila anaamini huuni msimu wa mpito kwao na ipo siku
mzunguko wa fedha utabadilika na kuweza kufanya bishara kwa kiwango cha juu na
kupata faida.
No comments:
Post a Comment