MWENYEKITI
wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,Kibena Kingo amesema hataruhusu mwekezaji
yeyote kupewa ardhi katika wilaya hiyo ikiwa bado wananchi wanaupungufu wa
ardhi kwa lengo la kupnguza migogoro ya ardhi.
Alisema
hayo katika tamasha la nne la jinsia
ngazi ya Wilaya 2016 lenye lengo la kumkomboa mwanamke kuwa na haki ya kumiliki
Ardhi,huduma bora za jami linalofanyika kata ya Mkambarani katika wilaya ya
Morogoro,kuandaliwa na TGNP Mttandao kwa kushirkiana na shirika la Action Aid.
Kingo
alisema kuwa wanawake wengi sehemu za vijijini hawajui thamani ya ardhi licha
ya kuitumia katika kuzalisha kila siku,ni wakati sasa wa kila mwanamke
kutafakari nafasi yake katika kumiliki ardhi.
“mimi
mwanamke kwangu ni wapi,ukimiliki hata hatua 10 za ardhi hapo ndiko kwako na
sio kuwaachia wanaume kumiliki ardhi na mwanamke unakuwa nyuma kila wakati”alisema
Kingo.
Aliwataka
TGNP mtandao na wadau wenginie kuendelea kutoa elimu ya umiliki wa ardhi hasa
sehemu za vijijini kunakofanyika mikataba hewa,hii ni kutokana na wananchi
wengi kuwa na uelewa mdogo juu ya sheria za kumili ardhi.
“wanawake
msipojitokeza kumiliki ardhi mtakuwa watumwa ndani ya nchi,jitokezeni katika
mikutano ya ugawaji wa ardhi inayofanyika kwa kufuata sheria na taratibu
zilizowekwa na seriakali”Aliongeza.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Kiloka,Robert Selasela alisema kuwa TGNP Mtandao
imewasaidia sana kutoa elimu kwa wananchi wa kata yake hasa katika kujitambua
na kujua haki zao za msingi na suala zima umuhimu wa kumiliki ardhi.
Selasela
alisema changamoto nyingi zimeibuliwa na wadau hao katika maeneo
mbalimbali,hivyo imewasaidia viongozi kupata matatizo ya wananchi wao kwa
karibu sana na hata kabla ya kufanya ziara ndani ya kata zao.
No comments:
Post a Comment