![]() |
Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini,Abdulazizi Abood akikabidhi mabomba ya kusambaza maji katika mtaa wa Magereza kata ya Kihonda Manispaa ya Kihonda. |
VIONGOZI wa serikalia za mitaa na kata katika
manispaa ya Morogoro wametakiwa kusimamia miradi ya maendeleo na kuweka siasa
pembeni ili wananchi wa chini kuweza kufaidika na matunda ya serikali yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Morogoro
mjini,Abdulaziz Abood wakati akikabidhi mabomba ya kupitisha maji katika Kata
ya Kihonda mtaa wa Magereza ambapo alisema thamana ya miradi ya maendeleo ya
serikali ipo mikononi mwa viongozi wa serikali za mitaa na kata.
Alisema kuwa miradi yote lazima iwe
inatembelewa na viongozi wa eneo husika na kuweza kuangalia mwenendo mzima na
kuweza kutoa taarifa kwa viongozi wa juu endepo kuna tatizo ili kuweza
kufanyiwa kazi na sio kuacha mpaka wananchi kuanza kulalamika na kuandamana.
Abooda alisema tatizo la maji katika manispaa
ya mororgoro hususani kata ya Kihonda litamalizika kwania serikali
imeshajipanga kushiriakiana na wafadhili na idara ya maji kuhakikisha wananchi
wake hawapati shida ya maji safi na salama.
Aliwataka viongozi na wananchi wa mtaa wa
magereza na jirani ambapo mabomba hayo yatasambazwa kwa ajili ya kusambaza maji
katika maeneo yao kuwa walinzi na kuhakikisha yanakuwa katika mazingira salama
kila mara.
Nao wakazi wa Mtaa wa Magereza kata ya Kihonda,walisema
kuwa jitihada zinazofanywa na mbunge Abood na serikali zitasaidia kupunguza kero
ya maji iliyokuwa inawatesa kwa kipindi
cha miaka mingi na kufanya kushindwa kufanya shughuli nyingine za
uzalishaji na kutafuta maji.
No comments:
Post a Comment