![]() |
Meya wa Manispaa ya Morogoro,Pascal Kihanga akikata utepe kufungua ofisi ya Kampuni ya Smile Communication mkoani Morogoro. |
WAKAZI wa Manispaa ya Morogoro wametakiwa kutumia huduma
zinazotolewa na huduma
za mawasiliano katika
kupata taarifa mbalimbali ikiwemo za kibiashara ili
kufanya shughuli zao kirahisi na ufanisi zaidi kwa lengo la kujipatia
maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Morogoro,Pascal Kihanga wakati akifungua Duka la Smile mjini Morogoro,ambapo
alisema huduma hiyo ya mawasiliano itaaidia sana kuleta maendeleo ya watu
binafsi na masnipaa kwa ujumla.
Kihanga alisema kuwa wakazi wa manispaa ya Morogoro sasa
wataweza kunufaika
na huduma zinazotolewa na kampuni hiyo na
hivyo kuwaletea mapinduzi mapya ya kasi ya internet kupitia mitambo ya
Smile 4G LTE .
Kihanga alisema kupitia huduma zinazotolewa na kampuni
hiyo itakuwa
faraja kwa wananchi hususani wafanyakazi ,wafanyabiashara na kwa matumizi
ya nyumbani wakiwemo wanafunzi ambao
wataweza kutumia huduma ya mtandao utakaowarahisishia kutuma na kupokea taarifa. .
‘’Sasa wafanyabiashara na hata wakulima wanaweza kunufaika na
huduma za mtandao uendao
kasi katika kupata taarifa mbalimbali za masoko na hata kibenki.’’alisema.
Kwa upande wake Meneja wa Mkoa wa Morogoro na Dodoma wa Kampuni
hiyo Zephania Mgonella alisema kuwa katika
sekta ya mawasiliano hapa
nchini Tanzania intaneti ya 4G LTE kwa sasa ndio inayoongoza kwa sasa kwa kuwa na kasi mara sita zaidi kuliko 3G na mara
nne zaidi kuliko 3.75G.
Mgonella alisema kuwa kupitia teknolojia hii wananchi
wa Morogoro wana uhakika
wa kasi ya upakuaji na kasi ya upakiaji wa mafaili ,barua pepe,nyimbo na
michezo ,matumizi ya
nyenzo mbalimbali za
kwenye mtandao na kwa
kuangalia video na televisheni bila kugomagoma.
Hata hivyo alisema kuwa Kampuni ya Smile ilianza rasmi mwaka
2012 na tayari imefungua matawi yake katika Mkoa wa Dodoma,Daressalaam,Mwanza
,Arusha ,Moshi,Mbeya na
hatimaye Morogoro kwa sasa.
No comments:
Post a Comment