JUMLA ya shilingi milioni 240.5 zimetolewa kwa
Kaya 6931 katika Wilayani Gairo mkoani Morogoro kutoka Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii(TASAF) huku kaya 124 zikitolewa katika mpango huo kwa kukosa vigezo.
Mratibu wa TASAF,wilaya ya Gairo,Annajoyce Rubagumisa alisema zozezi hilo limefanyika
kwa awamu ya sita sasa,na walifanikiwa kutoa fedha kwa wale wote waliokidhi
vigezo na 124 waliondolewa kutokana na kutokuwa na vigezo vilivyowekwa.
Alisema lengo la kutoa
hela ni kuziwezesha kaya maskini kuongeza kipato na fursa za kuboresha
upatikanaji wa mahitaji muhimu,na wanashirkiana na viongozi wa serikali za
vijiji kuhakikisha ruzuku hizo zinakwenda kwenye matumizi sahihi.
Rubagumisa
alisema jumla ya vijiji 50 vimepatiwa ruzuku hiyo,na kaya 124 ziliondolewa
kutokana na kubainika kuwa na uwezo wa
kujitegemea katika maisha yao.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Chamkobwe kata ya Chagongwe,Gadson James
alisema mpango huu wa serikali wa kuangalia kaya maskini unasaidia sana
wananchi kuweza kujimudu kimaisha na wengine kuwekeza katika kilimo.
James
alisema kaya zilizopatiwa ruzuku hiyo huwa wanawafuatilia kuangalia matumizi ya
fedha hizo na kuona ziko katika matumizi sahihi na wengi wao wamebadilika kimaisha.
Nae Mkazi
wa Chamkobwe,Happness Eliakimu,aliishukuru serikali kwa kubadili maisha ya
familia zao,kwani wameweza kuwanunulia watoto sare za shule,kupeleka shamba,pia
aliiomba serikali kuendelea kutoa ruzuku kwani kwa kufanya hivyo inajiimarisha
kwa wananchi wake.
Mwisho.
![]() |
Kijiji cha Chamkobwe kata ya Chagongwe wilayani Gairo wakisubiri kupewa ruzuku ya TASAF. |
No comments:
Post a Comment