Wednesday, April 6, 2016

SERIKALI KUENDELEZA SERA YA KILIMO KWANZA

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA),Prof.Gerald Monela wakikabidhiana hati ya makubaliano ya utoaji wa elimu ya kilimo kwa kutumia zana za kilimo na Mwakilishi wa kampuni ya John Deer,Lucas Botha 

SERIKALI imesema itaendeleza sera ya Kilimo Kwanza na kuhakikisha mkulima anaondokama na kilimo cha jembo la mkono kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa mazao yatakayotumika katika  viwanda vya hapa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa Mwishini mwa wikia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Dr.Florens Turuka katika uzinduzi wa mpango mpya wa Uashirikiano baina ya taasisi za umma na binafsi kwa ajili ya kuendesha mafunzo bora ya zana za kilimo uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.(SUA).

Dr.Turuka alisema zana za kilimo bado  zinahitaji na hivyo ni wakati wa sekta binafsi kutumuia nafasi hiyo kuweza kumsaidia mkulima na mjasiariamali kuweza kuzalisha kwa wingi ili sekta ya viwanda inavyokuwa isikije kukosa mali ghali ama kutegemea kutoka nje.

Kwa upande wake,Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA),Prof.Gerald Monela alisema SUA wakishirikiana na mradi wa ubunifu katika utafiti wa kilimo (iIAGRI) na kampuni ya zana za kilimo ya John Deer wamezindua mpango wa matumizi bora ya trekta na utafiti.

Prof.Monela alisema mpango huo unalengaa kutoa elimu ya vitendo kwa wakulima kwa minajili ya kuongeza uzalishaji kwa njia bora ya zana za kilimo,elimu itakuwa inatolewa kwa wakulima na wamiliki matrekta kutoka pande zote  Tanzania.

Nae Mkurugenzi wa mradi wa Ubunifu katika utafiti wa Kilimo,(iAGRI)Prof.David Kraybill alisema mradi unalenga kuandaa kizazi kijacho cha viongozi wa kilimo katika taasisi za umma na za binafsi  na kuimarisha taasisi mahususi za utafiti  na mafunzo ya kilimo nchini.

Kraybill aliongeza kuwa mradi huo unaandaa wahadhiri,watafiti,maafisa ugani na wanafunzi katika kuboresha mbinu za kutatua matatizo ya wakulima wadogo na wale wanaofanya biashara kilimo.


No comments:

Post a Comment