SEIKALI imeagiza halmashauri zote nchini kuwakati kadi za bima
ya Afya wazee wote wenye umri kuanzia miaka 75,na kupatiwa huduma ya vipimo vya
magonjwa yote bure pamoja na kuhimiza kutenga dawati maalumu la kuhudimia wazee
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na watoto,Ummy Mwalimu katika uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa
Mzee Kwanza Toa Kipaumbele apate Huduma iliyofanyika mkoani Morogoro.
Sambamba na hilo,Waziri Ummy ameuagiza Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya kuwalipia wazee 50 kwa kila Halmashauri
nchini kuweza kupata kadi za bima ambazo wataweza kuzitumia katika kuapata
huduma za afya katika vituo vya afya na zahanati.
Mwalimu alisema lengo la kampeni hiyo ni kuikumbusha jamii ya
watanzania kuhusu wajibu wa kuwapa wazee hadhi wanayostahili katika maeneo
mbalimbali ya huduma za kajamii.
Alisema serikali kupitia wizara ya Afya imeandaa muswaada wa
kutungwa kwa sheria ya wazee ambayo itapelekwa bungeni ili ipitishwe kuwa
sheria ambayo itasimamia upatikanaji wa haki na ustawi wa sheria ya wazee.
Pia alizitaka halmashauri zote kubaini wazee walio katika maeneo
yoa na kuhakikisha wanapata huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na huduma za
afya kutoka kwenye mapato yao wenyewe na viongozi wote wa halmsahuri kusimamia
zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya(NHIF),Michael Mhando alisema kuwa mfuko umetambua mchango mkubwa wa wazee
katika taifa,na wanaungana na serikali kuhakikisha wanapata huduma bora muda
wote.
Mhando alisema toka kuanzishwa kwa mfuko huo mwaka 2007 wamekuwa
wakitoa huduma kwa wazee kupitia kadi za bima,na wanaendelea kweka mazingira
mazuri katika kuhakikisha wazee wote wanahudumiwa vizuri katika sekta ya Afya.
Naye Mwakilishi wa Taasisi ya Help Age International,Danie Smart
alisema hakuna nchi inaweza kuendelea bila kujali wake hususani wazee,hivyo
jambo linalofanywa na NHIF na serikali kuzindua kampeni ya kuwaseme wazee
linapaswa kuungwa mkono na watanzania wote.
Smart alisema katika tafiri zilizofanyika hivi karibuni katika
masula bora ya Afya iliyoshirikisha nchi 96,Afrika kulikuwa na nchi 11 na
Tanzania imeshika nafasi ya 2 katika kutoa huduma bora za kiafya kwa wananchi
wake,na nafasi ya kwanza ikishilikiliwa na Mouritoius.
No comments:
Post a Comment