MBUNGE wa Jimbo la Morogoro mjini,Abduaziz Abood amesema
atatengeneza darasa moja katika shule ya msingi Lugala iliyopo kata ya Mindu
baada ya wanafunzi kukaa kwa mwezi mmoja kwa kukosa darasa kutokana na shule
hiyo kuanguka.
Akizungumza na wakazi wa mtaa wa Lugala na wanafunzi,Abood
alisema ili wanafunzi waendelee kupata elimu na kuachaku kaa nyumbani
atatengeneza darasa moja ambalo litatumika kusomea huku wakisubiri taratibu
nyingine kutoka kwa tume iliyoundwa manispaa kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Abood alisema mkandarasi aliyesimamia ujenzi wa shule hiyo
lazima ahojiwe na timu yake yote kutokana
na ujenzi kuonekana haukuwa imara na haukufuata vigezo vinavyotakiwa ndio maana
shule hiyo ilianguka na kusababisha hasara kubwa.
Pia aliwataka wakazi wa mtaa wa Lugala iliyopo shule hiyo
kufanya usafi katika mazingira yanayozunguka shule hiyo ili wanafunzi kuweza
kusoma katika mazingira salama,na kujitolea katika shughuli za maendeleo ya
ukarabati shule hiyo pamoja na kuhakikisha matundu ya choo yanakuwa salama kwa
watoto.
Kwa upande wake Mwalimu wa shule hiyo,Antony Shayo alisema kuwa
anashukuru jitihada za mbunge za kujitolea kutengeneza darasa hilo,pia watoto
waliokuwa wanakaa chini ila mbunge alijitolea madawati 40,kutokana na shule
kuanguka walikosa sehemu ya kuweka ila darasa likikamilika wanaamini watapata
madawati hayo.
Shayo alisema kuwa shule hiyo ilianza februari 2016,ina jumla ya
wanafunzi 85,huku ikiwa na walimu wawili wanaojitolea kufundisha,na darasa
likikamilika itabidi waongeze muda wa ziada wa wanafunzi ili kuendana na mtaala.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Lugala,Sanga Mkulago
alisema kuwa waliohusika katika kusimamia ujenzi wa shule hiyo wakiongozwa na
mtendaji kata hawafai,na watakaobainika kurubuni mradi huo wachukuliwe hatua za
kisheria kwani kuhamishiwa mtaa mwingine wataharibu kama walivyofanya Lugala.
![]() |
Mbunge wa Morogoro mjini,Aziz Abood akiongea na wananchi na wanafunzi wa shule ya msingi Lugala iliyoanguka na wanafunzi kukosa sehemu ya kusomea. |
![]() |
Mbunge wa Morogoro mjini,Aziz Abood akikagua jengo la shule ya msingi Lugala iliyopo kata ya Mindu iliyoanguka kutokana na ujenzi wake kuwa hafifu. |
No comments:
Post a Comment