KAYA zaidi ya 350 katika kijiji cha Mambegwa kata ya Msowero
Wilayani Kilosa zimeifadhiwa katika shule ya msingi Mambegwa kufuatia nyumba
zao kujaa maji na nyinginne kuanguka kutokana na mvua zinazonyesha.
Wakizungunza na wahabari,waathirika wa tukio hilo walisema kuwa mvua
hizo zimeanza kunyesha kubwa na upepo mkali mnamo tarehe 19/04,na kusababisha
maji kujaa ndani huku nyumba zikianguka na kukosa makazi ya kudumu.
Mmoja wa waathirika,Lucy Cosmas alisema kuwa hivi sasa hawana
chakula,watoto wanahaingaika njaa huku wwao wakishindwa kwenda shambani na
kufanya shughuli za uzalishaji kutokana na maeneo yote kujaa maji.
Cosmas aliiomba wadau na serikali ya wilaya na mkoa kusikia
kilio chao kwani hawana pakukimbia na hapo shuleni walipo hawajui watakula nini
na watoto watasoma katika mazingira gani kwani chakula walichopewa cha msaada
na serikali ya wilaya kimeharibika na kingine kuchukuliwa na maji ya mvua.
Jackson Mchome alisema kuwa eneo kijiji cha mambegwa
wamezungukwa na wawekezaji katika maeneo yote salama na kuiomba serikali
kuangalia uwezekano wa kuchukua mashamba pori na kugawa kwa wananchi ili
kuondokana na adha ya mafuriko wanayopata kila msimu wa mvua.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Mambegwa,Said Ally
alisema kuwa kaya zaidi ya 355 hazina mahali salama za pakuishi,huku mvua
zikiendelea kunyesha na kukaa na serikali ya kijiji na kuwachukua wananchi
kuwaweka katika shule ya msingi Mambegwa kwa usalama zaidi.
Ally alisema ameshatoa taarifa katika serikaliya kata na wilaya
hivyo wanasubiri maamazu hayo,kwani chakula kilichotolewa na serikali ya wilaya
tani 10 na kugawa kwa wananchi kimezombwa na maji na hivi sasa hawana chakula
na hawawezi kwenda mashabani kutokana na kijiji kizima kujaa maji.
No comments:
Post a Comment