Mkuu wa mkoa wa Pwani,Evarist Ndikilo na Meneja wa Usambazaji wa Kampuni ya M-Power Alfred Kohi wakikata keki kwa ishara ya upendo katika ufunguzi wa ofisi ya Kampuni ya M-Power mkoa wa Pwani.
SERIKALI imesema itaendelea
kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanaowekeza katika sekta ya umeme hapa nchini
ili wananchi wake hasa wanaoishi maeneo ya vijijini kuweza kupata nishati hiyo
na kupata huduma bora kwa wakati wote.
Kauli hiyo imetolewa na
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Evarist Ndikilo wakati akifungua ofisi za Kampuni ya
M-Power inayosambaza umeme wa jua katika kata ya Mkuza,ambapo alisema serikali
inaunga mkono wawekezaji wote wanaowekeza katika kusambaza nishati ya umeme.
Alisema serikali
imejipanga kuhakikisha wananchi wote wanaoishi vijini wanapata nishati ya
umeme,na hasa maeneo ambayo tanesco haijafika wanakaribisha wadau wa umeme
kujitokeza kwa wingi kuweza kusambaza nishati hiyo.
Kwa upande wake,Meneja wa
Usambazi wa Kampuni ya M-Power,Alfred Kohi alisema kuwa kampuni hiyo ilianza iina
miaka 4 hapa nchini na hivi sasa wameshafikia wateja zaidi ya 100,000 katika
mikoa 14 ambapo tayari wameshafungua ofisi na kuanza kazi ya usambazaji wa
umeme wa jua.
Kohi alisema lengo la
usambaza umeme wa jua ni kuhakikisha wananchi wa maeneo ya vijijini na mijini wanaotumia
mafuta ya taa kuweka kwenye kibatari kuondokana na adha hiyo na kuweza kutumia
umeme wa bei rahisi unaosambazwa na kampuni hiyo
Alisema kuwa kampuni
imejipanga na kuhakikisha mpaka kufikia 2017 wanakuwa na wateja zaidi ya
milioni 1 nchi nzima na kuhakikisha wananchi wa pembezoni mwa miji wanaondokana
na matumizi ya mafutaya taa ambayo yanasababisha magonjwa ya macho na kukuhoa
kutokana na moshi wa kibatari.
Pia alisema wanatoa huduma
kwa vituo vya afya na vituo vya polisi vilivyo pembezoni mwa mji ambavyo
havijafikiwa na nishati ya umeme wa tanesco kwa kuvifungia mtambo wa umeme wa
jua bure ikiwa ni kutambua umuhimu wa huduma zinazotolewa na vituo hivyo kwa
wananchi
Nae mkazi wa kata ya
Mkuza,Salum Rajabu alisema kuwa huduma iyosambazwa kamapuni ya M-Power ni bei
nafuu na wananchi wa kipato cha chini anaweza kumudu na kuomba seriakali na
wadau wengine kuwaunga mkono pindi wanapofika katika maeneo yao kutoa huduma.
|
No comments:
Post a Comment