Wilaya za
Kilombero,Kilosa ,Morogoro na Mvomero
zimetajwa kukithiri kwa
matukio ya kughushi saini na majina ya
wakulima katika vijiji katika
zoezi la ugawaji wa mbolea za pembejeo kutokana na mawakala na watumishi
wa srikalini kutokuwa waaminifu na
uadirifu .
Hayo yamesemwa jana
na mwenyekiti wa mtandao wa habari za kijamii Tanzania (mhakita)Bi
Merina Robart wakati akiongea na wanahabari kwenye majumuisho
ya ziara fupi katika
wilaya za mkoa wa Morogoro kuchunguza malalamiko ya wakulima kuhusiana na usimamizi
mbovu pamoja na hujuma katika
zoezi la ugawaji ruzuku za pembejeo.
Bi Merina
alisema kuwa katika ziara
fupi ya mhakita katika baadhi
ya wilaya imebaini wilaya hizo
nne zimekithiri kwa matukio
ya wizi wa ruzuku za pembejeo
kwa wakulima kwa
kughushi ,majina ya wakulima ili
kujipatia fedha nyingi pasipo kusambaza pembejeo katika vijiji.
Alisema kuwa
matukio ya aina
hiyo mhakita haitakuwa tayari kuyanyamazia
,kwa kuwa ni matukio
ya kuhujumu taifa kushindwa
kufikia malengo yake
ya uzalishaji kwa wakulima kutokana na hujuma
hizo za mawakala
wa pembejeo.
Hata hivyo
mwenyekiti huyo alisema kuwa
katika baadhi ya
vijiji wamekuwa wakiwataja watumishi wa
serikali waliokula njama na mawakala
katika kulazimisha kughushi saini na majina ya
wakulima katika maeneo yao .
“majina ya mawakala waliojihusisha na
zambi hizo tunayo pamoja na watumishi wa
serikali yapo itakapofikia hatua
ya kuwataja ili serikali ifanye
kazi yake tutayataja kwa
kuwa yamesemwa na
wakulima katika maeneo yao “alisema mwenyekiti huyo.
Alisema kuwa
kazi za asasi zisizo za kiserikali ni kuisaidia
serikali kuhakikisha mipango na
sera za serikali zinatekelezwa kw a umakini ili
kuepusha serikali kuingia
katika hasara kubwa
katika miradi yake .
Mwenyekiti huyo alidai kuwa mhakita
kama mdau wa serikali katika
kuimiza maendeleo ya jamii bila
kujali itikadi za kidini , siasa imekuwa
mstari wa mbele katika kufichua maovu yeyote yenye lengo
la kukwamisha jitihada
za serikali katika kuhakikisha
jamii inapata maendeleo ya kasi kubwa
katika maeneo yao.
Hata hivyo
amedai kuwa mhakita ni asasi yenye wigo mkubwa
wa kufanya kazi katika mikoa
yote Tanzania bara itaendelea kutoa ushirikiano kwa serikali
katika maeneo mengine ili kuakikisha serikali inafikia malengo yake
katika sekta mbalimbali nchini
Alisema
kuwa wilaya hizo nne mkoani Morogoro zimekithiri matukio hayo ya
ubadhirifuna ulaghai kutokana na uzembe
wa watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia zoezi zima
la ugawaji wa ruzuku za pembejeo .
Hata hivyo
mwenyekiti huyo ameiomba serikali na
taasisi nyingine kuiunga mkono
mhakita ili kufanikisha kufikia
malengo yake ya
kuandika habari za kijamii zaidi
hususani vijijini ambako kumekuwa
na uhabarishwaji wa habari za matukio
ya wananchi “mhakita imekusudia kufanya kazi za kihabari na jamii hasa vijijini”alisema Bi Merina .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment