Thursday, May 2, 2013

RC MOROGORO AONYA MADIWANI WENYE MAJUNGU


MOROGORO .
Mkuu  wa mkoa  wa Morogoro ,Bw Joel Bendera  amewataka  madiwani  wa halmashauri  ya Manispaa  ya Morogoro kuacha  majungu na badala  yake  kutekeleza yale  walioahidi  kwa  wananchi  katika maeneo yao.
Bw Bendera  alisema hayo  jana  kwenye  kikao cha kawaida cha  baraz a la madiwani wa halmashauri  ya manispaa  ya  morogoro  mjini ,alipokuwa akiongea  nao kuhusu  umuhimu wa kusimamia sera  na  utekelezaji wa ilani  ya chama  kilichowaweka madarakani .
Alisema  kuwa yeye  kama mkuu  wa mkoa  wa morogoro anakelwa  kuona  kuwa  madiwani waliopewa  dhamana  ya  kusimamia  utekelezaji wa ilani  na sera  wamekuwa wakipingana katika mambo  ya msingi  ndani  ya manispaa .
Mkuu  huyo  wa mkoa  alisema  kuwa anakerwa  kuona  kuwa wapo  baadhi  ya madiwani wamekuwa mabingwa wa  kupeleka majungu  ofisini kwake  lakini , pia   hao  hao wamekuwa  wakipingana na baadhi  ya  maamuzi mazuri  wanayopanga  kwenye  baraza  la madiwani  kwa lengo  la kubadilisha mazingira  na taswira  ya  mji  wa morogoro  kufikia  kuwa  na hadhi  ya kuwa  jiji.
“Nimechoshwa na wanaokuja  ofisi  kwangu  kuleta majungu ,sasa  hivi  ukileta  majungu nakufukuzia mbali nataka  uje  na mipango  ya  kuibadilisha morogoro”alisema  mkuu  huyo  wa mkoa .
Aidha  alisema  kuwa  mpango wa manispaa  ya Morogoro  ni kuhakikisha  kwa mjini  unakuwa  katika  hali  ya usafi  na kuondokana  kabisa  na  biashara  za barabarani kama ilivyo sasa hivi,kila  kona  kumekuwa na  wafanyabiashara  wadogo.
Alisema  kuwa  ni jambo  la  aibu  kuona  kila  kona  kumejaa  biashara  za barabarani   kwani   kuwa  ndio chganzo  cha mji   wa morogor  kuonekana  mchafu na kushindwa  kufikia  malengo  ya  kuwa  na hadhi  ya kuitwa  jiji .
Hata  hivyo mkuu  huyo  wa mkoa  ameitaka  halmashauri  ya manispaa  ya Morogoro  kuimalisha askari  mgambo na askari  polisi ili kuhakikisha wanasimamia  zoezi  la kuweka  mji safi siku  zote  na  sio  kwa muda  tu .
Aidha  pia  ameiomba  halmashauri hiyo kuakikisha  wanawaa ndalia  sehemu  nzuri  wafanyabaishara  wote  watakaoondolewa  barabarani  ili  kuwafanya  wavutike  kukaa  katika maeneo wanayoamishiwa  kibiashara .
Aidha naye  mstahiki meya  wa manispaa  ya Morogoro , Bw  Amir  Nondo  akijibu  maekelezo  ya mkuu  wa mkoa , alisema  kuwa  halmashauri  yake  imepania  kushika nafasi  ya  kwanza  katika mashindano  ya miji  yenye  sifa  za usafi na  kutoka  kwenye nafasi  ya  12   walioshika  mwaka  jana .
Alisema kuwa  atakuwa mstari  wa mbele  kusimamia  zoezi  hilo  kwa kushirikiana na watumishi wa  halmashauri   wote  kuanzia mitaa  , kata  na  tarafa  ili  mradi  kufanikisha malengo  ya  kuweka mji  kuwa  katika  hali  ya  usafi
mwisho

No comments:

Post a Comment