Saturday, April 20, 2013

TUICO YATUNUKU WANANCHAMA SITA UANACHAMA WA HESHIMA,AKIWEMO INJINIA STELLA MANYANYA.

        
                                          Mwenekiti wa TUICO,Omary Ayoub akimkabidhi Injinia Stella Manyanya cheti  cha uananchama wa heshima katika chama hicho.

CHAMA cha wafanyakazi  wa viwanda,biashara  Taasisi za fedha ,huduma na ushauri (TUICO) kimewatunuku jumla wanachama  sita uananchama wa  ya heshima   kupitia kikao cha Baraza kuu la chama hicho.

 Katibu Mkuu Msaidizi sekta ya biashara Peres Jonathan alisema kuwa hiyo imetokana na mwongozo wa chama hicho kwa mujibu wa sheria sura nambari 3 .1 hadi 3.3,ambapo inataka waasisi,wanachama waliojitolea kukiendeleza chama wanaweza kutunukiwa uanachama wa heshima

Jonathani aliwataja waliotunukiwa uanachama wa heshima kuwa ni pamoja na Mhe.Felister Bura, Prof Issa Shivji Injinia Stella Manyanya,Wakili Julius KalolonBundala,Balozi Alfred Tandau na Zephani Sumbe,lengo kuu ikiwa ni kutambua mchango wao ikiwa ni pamoja na kutumia ujuzi wao

Alisema kuwa lengo kuu la kuwatunukua wanachama wa heshima  ni kutambua mchango wao mkubwa walioufanya ikiwemo kuwafanya kuendelea kutumia ujuzi,uzoefu wao wa haki na busara katika kukiendeleza chama cha TUICO kwa muda mrefu bila kukata tama kwa kila jambo linalotakiwa ufafanuzi

‘’Kwa kuthamini mchango wao walioufanya na watakaoendelea kuufanya ndio maaana wanachama wote wa TUICO  kupitia Mkutano mkuu Mkoni Tanga waliazimia na   kuwatunuku siku ya leo rasmi  na ni matarajio yetu kuwa heshima hii  tuliyowapa itasaidia na kukiimarisha chama chetu kwa  aufanisi mkubwa na kuleta tija tuliyoikusudia’’alisema Bw. Jonathan.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dares salaam Prof,Issa Shivji alisema kuwa TUICO imeweza kutataua changamoto mbalimbali hususani katika sekta ya viwanda na biashara katika suala zima la wafanyakazi na hivyo kutoa wito wa wafanyakazi wa viwanda kuungana kwa pamoja ili kuunganisha nguvu katika kutetea maslahi yao .

Shivji alisema kuwa wafanyakazi wengi wa viwandani  wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ya kunyonywa na waajiri wao  ikiwemo kufanyishwa kazi  muda mrafu  na kutolipwa mishahara kwa wakati muafaka na kutodhaminiwa katika utendaji wao.

‘’Ni wakati sasa  kwa wafanyakazi wakaungana kikamilifu ili kuhakikisha tabia hii inakwisha au kutokomezwakabisa kwani inarudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa kuendelea kuwanyonya wafanyakazi ‘’aliongeza Prof.Shivji. 
Mwenyekiti wa TUICO taifa,Omary Ayoub Juma alisema kuwa wako tayari kufanya kazi kwa ukaribu na  watumishi hao waliotunukiwa nishani ya heshima na pale ambapo wataona wanaenda kinyume na katiba na sheria wakosolewe bila kuonewa aibu

Ayoub alisema  ni vyema uanachama waheshima ikawa chachu kwa taifa katika kuhakikisha kila mtumishi au mfanyakazi yoyote anafanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa huku akithaminiwa kikamilufu na mwajiri kwa kutambua uzalishaji wake katika taifa.
Mwisho. 

Wanachama wa TUICO waliotunukiwa vyeti vya uanachama wa heshima wa chama hicho katika mkutano mkuu uliofanyika mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment