Viongozi wa Wezesha Trust Fund wakifurahi na watoto |
Mkurugenzi wa Wezesha Trust Fund Lusako Mwakiluma akitoa zawadi ya vyakula na vitu mbalimbali katika kituo cha kulea watoto Dar-UI-Muslimee kilichopo kata ya Mbuyuni Manispaa ya Morogoro |
VITUO vitano vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu vya Amani Center,Dar-Ul- Muslimee Center,Bigwa Center na EGT Sayuni vyote vya mjini Morogoro vimepatiwa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 1 milioni kwa ajili ya sikukuu ya pasaka.
Akikabidhi misaada hiyo mkurugenzi wa Wezesha Trus Fund ya mjini hapa Lusako Mwakiluma alisema kuwa wamehamua kutoa misaada hiyo kwa watu h wenye mahitaji kutokana na kusahalika katika jamii na kwamba misaada hiyo itawasaidia kuwafanya wafurahi hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka.
Mwakiluma alivitaja vitu vilivyotolewa kuwa ni pamoja na Sukari,Mchele,Mafuta ya Kula,Sabuni ya kufulia,unga wa ngano,juisi,samaki na nyama.
Aidha mkurugenzi huyo aliyataka mashirika na watu binafsi kujitokeza kutoa misaada kwa watoto hao ili kujengea imani ya kutoona kama wanatengwa katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya vituo vingine msimamizi wa kituo cha Dar Ul muslimeem center Maulid Omary alishukuru kwa misaada kama hiyo ambayo imekuwa ikisadia watoto kujikimu katika mahitaji yao ya kila siku.
Omary alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa chakula,madawa,mavazi na malazi ambapo aliimba serikali kusaidia kutatua kero hizo ikiwa ni pamoja na kuwajenga watoto.
No comments:
Post a Comment