Saturday, February 2, 2013

WAHANDISI KILOSA WALALAMIKIWA KUFANYA KAZI KWA SIMU


KILOSA .
Waandisi    wa  maji  katika  wilaya  ya Kilosa  wamelalamikiwa kubweteka ofisini  na   kufanya  kazi  kwa  njia   ya simu,hali ambayo  imekuwa  chanzo kikubwa  cha ujenzi  wa  miradi  isiyo  na ubora  katika  wilaya  hiyo .
Wakiongea na  waandishi wa habari mara  baada  ya mkutano wa  wadau wa  sekta  ya maji  katika  tarafa  ya  Gairo mkoani morogoro , ulioandaliwa  na asasi  isiyo  ya  kiserikali  ya  Kijogoo Group for community development iliyofadhiwa na  shirika lisilo  la kiserikali  la The  Foundation Civil society .
Wakazi  hao wamedai  kuwa  waandisi   wa maji  katika  halmashauri  ya  wilaya  ya  Kilosa  wamekuwa  chanzo  kikubwa  cha upotevu wa  fedha  za serikali  kwa kushindwa  kusimamia miradi  ya maji   kikamilifu  na badala  yake  usimamia  miradi  kwa  kutumia  simu za  mikononi.
Bw  Yusuph  Mkunda  mkazi wa kijiji  cha Kibedya tarafa  ya gairo amedai  kuwa wananchi wamekuwa wakipata  wasiwasi  juu  ya  waandisi  katika  halmashauri  hiyo  kutokana  na hali  halisi   ya wakandarasi waliopewa   tenda  ya kuchimba  visima , wamekuwa wakifanya kazi  chini  ya  kiwango.
Alisema  kuwa  visima   vingi  katika   vijiji  vya  Kibedya  ,Chakwele  , Gairo , Iyogwe  na Tabu Hotel  vimechimbwa    chini  ya  kiwango
Aidha  Bw  Mkunda  alidai  kuwa ni wazi  waandisi  hao  wamekuwa wakishirikiana na kandarasi  kufanya  hujuma katika   zoezi   zima  la  uchimbaji wa visima , ikiwa  pamoja  na  kuchimba  visima  chini  ya  kiwango kinyume  na maelekezo  ya  watalaam.
Hata  hivyo mkazi  huyo  wa  Kibedya  alisema  kuwa  mfano   wa  usimamizi  mbaya  wa miradi  ya  maji  katika  tarafa  ya  gairo  dhidi ya  waandisi , ni  kisima  cha  Kijiji  cha  Tabu Hotel , mkandarasi alitakiwa  kuchimba  kisima  kirefu chenye  piston  nne  lakini  katika  hali  ya kuchangaza mkandarasi  huyo aliweka  piston moja  na kusababisha kisima  hicho kushindwa  kufanya kazi .
“imani  inatutoka  kabisa  na  waandisi wa maji  katika  wilaya ya Kilosa   uwenda  wakawa  wanahusika moja  kwa moja  na  rushwa    kwa kushirikiana  na wakandarasi “ alisema  Bw  Mkunda .
Aidha  wakazi  hao wamedai  kuwa  wakandarasi wengi wamekuwa wakichakachua  zoezi la  uchimbaji wa  visima huku waandisi wa  halmashauri wakiendelea  kubweteka  maofisini  na  mkusimamia  miradi  ya maji  kwa  njia  ya  simu bila  kujua  serikali  imekuwa  ikipoteza kiasi  kikubwa  cha pesa  kutokana na  uzembe  wa  waandisi .
Walisema  kuwa   visima   vingi  vinavyochimbwa   katika  tarafa  ya  gairo  chini  ya  kandarasi  zilizopewa  tenda  vimekuwa   vikitoa maji  siku moja  tu na baada  ya  hapo  imekuwa  ni ndoto , hali ambayo wananchi wamekuwa wakihoji kazi  ya waandisi wa  maji wilaya  ya  kilosa ni kitu gani , zaidi  ya kuitia  hasara  serikali na halmashauri .
Hata  hivyo  katika maoni  yao  wananchi  katika  tarafa  ya Gairo wameiomba  ofisi  husika  kufanya  taratibu za  kua misha  waandisi  hao ambao wanadaiwa kukaa  katika  halmashauri  hiyo  kwa  zaidi  ya  miaka 20  hali ambayo  inawaladhimu  kufanya  hujuma  kutokana na kuizoea halmashauri  na watendaji wengine .
Wananchi hao  wamedai  kuwa  wamekosa  kabisa  ushirikiano na  mhandisi aliyeopo  katika  tarafa  ya  gairo katika mamlaka ya  maji ya mji mdogo wa gairo  katika  kutoa  taarifa mbalimbali kwa lengo  la kuboresha mindo mbinu.
“ mhandisi  wetu Bw Yakobo Mandago hatusaidii  kabisa kuhusu  suala  zima la uboreshaji wa huduma  ya  maji tunaomba  serikali inagalie   uwezekano wa kutusaidia juu  ya  mhandisi  huyu”alisema Bw fabia  Lumbiji makazi wa Chakwale , ambaye  ni  katibu wa kisima  cha maji .
Hata hivyo  juhudi za  kumpata  mhandisi Yakobo  Mandago  kujibu  tuhuma  hizo  zilikwama  na badala  yake  mwandishi wa gazeti  hili alifika  katika  ofisi  ya  halmashauri na  kukutana  na mhandisi ambaye  alijitambulisha  kwa  jina  la Bw  Abas ndeli na  na kudai  kuwa  yeye sio msemaji wa idara  ya  maji na  kudai  kuwa  mhandisi mkuu alikuwa  safarini  kikazi .
Mwisho.

No comments:

Post a Comment