Tuesday, January 29, 2013

TUNZENI MAZINGIRA-MTAKA


MKUU wa Wilaya ya Mvomero John Antony Mtaka amezitaka taasisi zisizo za kiserikali kuendelea kushirikiana na serikalia katika harakati za kuleta maendele hasa katika nyanja za utunzaji wa mazingira ambayo imekuwa kero kubwa kwa taifa

Mtaka alitoa mwito huo wakati akifungua mafunzo ya Ufugaji wa nyuki na utunzaji wa mazingira na misitu iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la  Asasi ya Blessing Group yaliyowashirikisha vikundi mbalimbali katika jamii kutoka tafara ya Turiani,katika vijiji vya Lungo,Madizini,Dihinda, Lusanga,Diongoya na Dori

Alisema kuwa mchango unafanywa na taasisi binafsi katika kuleta maendeleo ni mkubwa sana na serikali inawadhamini sana mchango wao na watakuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha zinakabiliana na changamoto zinazoikabili jamii kwa nyakati taofuti

“sisi serikali tutakuwa mstari wa mbele katika kutoa mchango wetu kwa taasisi binafsi hasa zile zinazopambana na utunzaji wa mazingira kwani uharibifu wa mazingira kunachangia mabadiliko makubwa ya tabia ya nchi”alisema Mtaka

Kwa upande wake Mwenyekiti Mtendaji wa  Asasi ya Blessing Group ,Aron Simon Mlemi alisema wameandaa mafunzo kwa wananchi juu ya kujenga uelewa  kwa jamii ambao ndio wadau wakubwa kushirki katika ufugaji wa nyuki kitaalamu na utunzaji wa mazingira na kila kijiji katika yatengwe maeneo maalumu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ili kufanikisha zoezi hilo
Alisema kuwa asasi kwa kwa kushirkiana na serikali wanahamashisha,kuanzisha na kuendeleleza ufugaji wa nyuki kwa njia za kisasa katika wilaya ya mvomero unaozingatia utunzaji wa maingira na utakaochangia kikamilifu kwenye uchumi wa wafugaji  ikiwa ni juhudi za kuhakikisha jamii inapata maendeleo endele endelevu

Mlemi alisema asasi pia inahamashisha ufugaji wa samaki,kuhimiza matumizi bora ya ardhi,matumizi bora ya misitu na bionuwai,kuanzisha vitalu vya miti na mazao mengine frafiki wa mazingira pamoja na kilimo chocheo cha utunzaji wa mazingira na kuhimiza uzalishaji wenye tija katika taifa

Alisema tatizo kubwa linalosumbua wilayani mvomero ni baadhi ya watu kuchoma misitu hovyo hasa nyakati za kiangazi maeneo mengi ya milimani,nah ii inatokana na kundi kubwa linategemea shughuli za uchomaji mkaa kama njia ya kujipatia kipato cha kila siku bila kujali kuwa wanaharibu mazingira

Kupitia mradi wa ufuagji wa nyuki pato litaongezeka kwa kiasi kikubwa lakini pia itaaidia katika kulinda misitu na utanzaji wa mazingira kwa faida ya vavyo kwani wafugaji wengi wa nyuki wanajikuta wameingia katika utunzaji wa mazingira kwani bila miti huwezi fuga nyuki na hakuna nayekubali shamba lake kuchomwa moto.

Alizitaja changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni kukosekana kwa elimu endelevu ya ufugaji wa nyuki kitaalamu kwa njia ya bora ya kisasa badala ya mizinga ya magome na magogo kwani hauna tija na kuchangia katika uharibifu wa mazingira

Nyingine ni asali huuzwa kabla ya kuchakatwa Wilayani Mvomero na mwingiliano mkubwa wa matumizi ya ardhi ambayo siyo rafiki kwa ufugaji wa nyuki kwa njia bora ya kisasa

 Hata hivyo alisema kuwa mradi wa ufugaji wa nyuki na utunzaji wa mazingira/misitu katika wilaya ya Mvomero umefadhiliwa na Tanzania forest Fund katika Kata ya Mtibwa,Mkindo
Mwisho

No comments:

Post a Comment