Morogoro .
Mamlaka ya
mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa
kushirikiana na jeshi la
polisi nchini wamejipanga vizuri
katika kukomesha uharifu
wa kwenye mitandao , kwa lengo la
kuwalinda watumiaji wa mawasiliano wanaolalamikia kukithiri
kwa vitendo vya uharifu
katika mitandao ya simu.
Hayo yamesemwa
jana na naibu mkurugenzi wa masuala
ya watumiaji wa mawasiliano (TCRA),Bw Richard Kayombo kwenye
mkutano wa wadau wa mawasiliano mkoani Morogoro,alisema kuwa ni
vyema jamii ikajua kuwa pamoja na matumizi mabadiliko ya technolojia lakini pia
wapo watu wamekuwa wakitumia mwa
nya huo
katika kufanya matukio ya
uharifu.
Bw
Kayombo alisema kuwa kuna makundi ya
watu wamekuwa wakifanya uharifu kwenye
mitandoa mbalimbali kwa kutumia majina ya
viongozi wakuu mbalimbali wa serikali kinyume
na sheria na taratibu.
Alisema kuwa kundi
hilo la matapeli limekuwa
likitumia majina ya
viongozi wa wizara ya kilimo
na kudai kuwa
wamekuwa wakiitaji shehena
ya madwa
ya kilimo , kumbe
ni uongo bali
ni njia za kutaka
kufanya utaoeli kwa mtu waliomkusudia .
Hata hivyo mammla
hiyo pia imewataka
watanzania kutokubali kirahisi
kila kitu wanachokikuta kwenye mitandao na badala
yake wajenge dhana
ya kuhoji katika
vyombo husika vinavyotajwa
katika mitandao .
Aidha alidai
kuwa wengi wao wanaotapeliwa ugundua mara
baada ya kubaini
kuwa wameibiwa ama
kutapeliwa ,”ni vyema jamii
ikaepukana na biashara za maghendo
ili kupu8nguza matukio
ya utapeli “alisema Kayombo.
Hata hivyo naibu mkurugenzi huyo alisema
kuwa ni vyema
jamii ikatumia simu
kwa madhumuni iliyotengenezwa badala
ya kugeuza simu
kuwa ni chombo
cha kufanya uharifu , kama wizi
na matusi .
Bw Kayombo
amewahakikisha watanzania kuwa kwa
sasa ushirikiano uliopo
baina ya mamlaka na jeshi
la polisi katika
kukomesha vitendo vya
uharifu katika vyombo
vya mawasiliano kama simu utasaidia kwa
kiasi kikubwa kuwanasa
waharifu wanaofanya uharifu
katika mitandao mbalimbali
ya mawasiliano .
Hata hivyo
naye katibu tawala
mkoa wa Morogoro , Bw Eliya Ntandu
akifungua mkutano huo
aliitaka mamlaka hya
mawasiliano kuendelea kuboresha
huduma hasa katika makundi yote
ya walemavu ili wapate
fulsa ya kutumia
mawasiliano pasipo usumbufu .
Bw Ntadu
pia alisema kuwa
bado kuna changamoto
nyingi katika mitandao
ya simu , ikiwa pamoja
na mitando kutuma ujumbe usiohitajika kwa mtumiaji
hali ambayo imekuwa kero kubwa kwa watumiaji .
Changamoto nyingine
ni pamoja na kukatika kwa mitandao
mara kwa mara
hali ambayo imekuwa kero
kubwa kwa watumiaji ambao
wamekuwa wakitumia zaidi mitandao kwa ajili
ya kuendesha shughuli mbalimbali
za uzalishaji .
mwisho
No comments:
Post a Comment