![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro,Mihungo Ruyemamu akiangalia risiti zilizotumika kuweka fedha benki katika akaunti ya kijiji cha mindu |
![]() |
Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Morogoro wakitembelea mgodi wa kuchimba mchanga katika kata ya Mindu. |
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood akiongea na wananchi wa Kata ya Mindu. |
WANANCHI wa Kijiji cha
Mindu Kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro wameiomba serikali ya Wilaya kubadili
uongozi wa serikali ya kijiji kutokana na utendaji mbovu wa viongozi hao pamoja
kutoa kauli chafu kwao pindi wanapodai haki zao za msingi.
Wakizungumza katika kikao
kilichojumuisha kamati ya Ulinzi na Usalama ya Morogoro,Said Mkmba alisema kuwa
watendaji hao wa kijiji wamekuwa wakiitisha mkutano na kusoma mapato na
matumizi ya fedha zikiwa hazijakamilika na hivyo kuzuka kutokuelewana na
viongozi hao kwa muda mrefu.
“Tunaomba waondoeni
viongozi hawa wa vijiji,hawatufai kabisa kutokana na utendaji wao pamoja na
kutoa lugha za matusi na vitisho kwa wananchi wanaodai haki zao hasa upande wa
matumizi ya fedha za miradi ikiwemo uchimbaji wa mchanga”Alisema Mkamba.
Zainabu Abdallah alisema
kuwa mradi wanaoutegemea katika pato la kijiji ni mradi wa uchimbaji wa mchanga
ambao wamewapa waekezaji wa ndani ila kinachosikitisha ni matumizi na mapoto ya
ushuru uliotozwa wawekezaji hauleweki unaenda wapi.
Kwaupande wake Mbunge wa
Jimbo la Morogoro mjini,Abdulaziz Abood
aliungana na wanachi hao na kusema kuwa uongozi huo unapaswa
kubadilishwa kutokana na kulalamikiwa mara kwa mara na wananchi katika utendaji
wao mbovu
Mkuu wa Wilaya ya
Morogoro,Mihungo Ruyemamu alimtaka mkurugenzi wa Manispaa kumuondoa mtendaji wa
kijiji cha Mindu,na kufanya hivyo ni pamoja kulinda usalama wake kutokana na
wananchi kutokuwa na imani nae kabisa.
Ruyemamu pia alimtaka
mkurugenzi huyo kushirikiana na kamati ya mazingira kuhakikisha eneo la mgodi
wa mchanga linakuwa na vyoo ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kutokana na wanachi
wanaochimba mchanga wanajisadia vichakani kwa muda mrefu.
Hata hivyo aliwataka
viongozi wa kijiji hicho kupeleka muhtasari za vikao,taarifa ya fedha ofisini
kwake ili kufanyiwa ukaguzi na wakaguzi wa ndani wa manispaa na kuahidi kutoa
taarifa ya ripoti hizo kwa wananchi hao pindi zitakapokamilika.
Nae Mtendaji wa kijiji cha
Mindu,Yusufu Ahmed alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya kijiji lakini
wananchi hawajitokezi hivyo kushindwa kujua miradi ya maendeleo ndani ya kijiji
inaesndeshwa aje na ipo katika hali gani.
Mnamo tarehe 10/12 wananchi
zaidi ya 30 kutoka kijiji cha mindu waliandamana hadi ofisi ya Mbunge wa Jimbo
la Morogoro mjini Aziz Abood wakidai kuondolewa kwa uongozi wa kijiji
waliowatuhumu kwa kuuza maeneo hovyo,ushuru wa mchanga na kutosomewamapato na
matumizi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment