SERIKALI
mkoani Morogoro imewataka walimu wa shule za msingi kuacha tabia ya kuwafaukuza
wanafunzi wanaokosa baadhi ya vifaa na sare za shue kwani jukumu la kuwanunulia vifaa hivyo ni wazazi na
walezi na kuendelea kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria
Kauli
hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero,Betty Mkwasa kwa niaba ya Mkuu wa
Mkoawa Morogoro,Dkt.Rajabu Rutengwe katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga
ukatili wa kijinsia zilizoandaliwa na Kituo cha Wasaidizi wa Sheria pamoja na
Dawati la Kijinsia kutoka kituo cha Polisi kwa udhamini wa WILDAF.
Mkwasa
alisema jukumu la kuhakikisha watoto wanasoma na kupata elimu bora ni wazazi na
walimu,hivyo ni jambo la aibu kuona mwalimu anamfukuza mtoto shuleni kwenda kwa
kukosa vifaa ama sare za shule badala ya kuwasiliana na wazazi wake kujua
taitozo liko wapi huku mwanafunzi akiendelea kusoma
Alisema
imefikia wakati sasa jamii kuondokana na dhana potofu ya kumsomesha mtoto wa
kiume na kumwacha wa kike,hii imepitwa na wakati kwani watoto wote wana haki
sawa ya elimu na serikali ya sasa itahakikisha watoto wote wanasoma bure bila
kusumbuliwa mashuleni
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Wasaidizi wa
Sheria,Flora Masoy alisema takwimu zinaonesha kwa kipindi cha mwaka 2015 kesi
za ukatili wa kijinsia zilizoripotiwa katika kituo chao zilikuwa 158,ambapo
watoto 38 wakiume na 120 watoto wa kike waliofanyiwa ukatili tofauti.
Masoy alisema amoja na jitihada zinazofanywa zinazofanywa na
serikali, vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vinakithiri katika jamii zetu,hivyo
sababu za makusudi zinatakiwa kuhamasisha
jamii kushiriki kikamilifu katika kuzuia ukatili wa Kijinsia kwani kwa
kiasi kikubwa jamii imekuwa ikichochea au ikikubali uwepo wa ukatili wa
kijinsia kwa kutokutoa taarifa au
kuchukua hatua kukemea ukatili wa
kijinsia.
Aidha
aliiomba serikali kuchukua hatua za makusudi kurekebisha Sheria
zinazohamasisha ukatili wa kijinsia,sababu zote zinazochangia watoto kukosa
haki ya elimu pamoja na kutungwa kwa
Sheria ya ukatili wa
kijinsia na adhabu kali zitolewe kwa
watu wanaohusika na ukatili wa kijinsia hasa wanaokatisha wanafunzi masomo.
Mwisho.
Wananchi wa Manispaa ya Morogoro,wakiwa katika maandamano ya kuadhiisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dunia. |
Mkurugenzi wa Kituo cha Wasaidizi wa Kisheria,Flora Masoy akisoma risala katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Morogoro zilizofanyika katika viwanja vya mashujaa. |
No comments:
Post a Comment