Thursday, April 17, 2014

LAPF,YAKUTANA NA WANAHABARI MJINI MOROGORO

Afisa  Matekelezo wa Mfuko wa jamii,LAPF,Charles Mahanga akiongea na wanahabari mjini Morogoro.


MENEJA wa Mafao wa Mfuko wa pensheni wa LAPF Kanda ya Mashariki Abubakari Ndwata amewataka waajiriwa wapya kuchukua tahadhari na taarifa mbalimbali ambazo siyo za kweli zinazotolewa na baadhi ya Mifuko ya hifadhi ya Jamii nchini ambazo zinalenga kuwarubuni ili wajiunge na Mifuko hiyo kinyume na taratibu zinazokubalika kisheria.

Akizungumza na wanahabari mjini Morogoro,Ndwata aliwataka walimu wapya watakaoajiriwa kuanzia tarehe 1/4/2014, watulie, wasikilize Mifuko yote katika halmashauri zao na hatimaye wachague bila kushurutishwa kujiunga na mfuko fulani na mtu yeyote kwani maamuzi wanayo wenyewe kwa mujibu washeria

Alisema kuwa walimu wanatakiwa kutambua kuwa mafao yanayotolewa na yapo katika makundi makuu mawili, yaani yale ya Mfumo wa hiari na mfumo wa lazima. Kwakuwa walimu wanaoajiriwa wanajiunga kwenye mfumo wa lazima, ni vyema wakadadisi kiundani kujua mafao wanayo ahidiwa yanatoka kwenye mfumo wa lazima

 Aliongeza kuwa kuna mifuko haina baadhi ya mafao katika mfumo wa lazima mfano fao la uzazi lakini wanaeleza kana kwamba wana fao la uzazi katika mfumo huu wa lazima jambo ambalo sio la kweli na wana nia ya kupotosha walimu na wananchi wengine

“vyema walimu wakapata fursa ya kusikiliza mifuko yote kabla ya kujiunga ambapo kwa taarifa zilizopo baadhi ya mifuko inawataka walimu kujiunga hata kupitia mitandao ya simu”alisema Ndwata.

Aliongeza kuwa wamepata taarifa nyingi za upotoshaji kutoka kwa baadhi ya watumishi wa mifuko mingine wakieleza kwamba wanatoa mafao kama ya uzazi kwa wanachama wao huku wakijua kwamba siyo kweli hata kidogo na sheria zao hazijasema hivyo,LAPF inasisitiza umakini katika kufanya uchaguzi sahihi na kwa taarifa zilizo za kweli.

Hata hivyo alisema kuwa LAPF itaendelea kujitangaza kwa kueleza ukweli wa yale ambayo inatoa na siyo ahadi hewa,kwa mfano, fao la uzazi LAPF imekuwa ikilitoa kwa wanachama wake kwa kiwango cha 129% ya mshahara na kwa kipindi cha miaka mitatu wanachama 3,252 wamenufaika na fao hili ambapo kiasi cha Sh 2,271,756,017.72 kililipwa.
                                         
Afisa  Matekelezo wa Mfuko wa jamii,LAPF,Charles Mahanga akiongea na wanahabari mjini Morogoro.



No comments:

Post a Comment