WANANCHI wametakiwa kutambua maoni yanayokusanywa ya kuunda katiba mpya ni kwa maslahi yao binasfi na sio kwa faida ya chama cha siasa kama baadhi ya wanachi wanvyofanya badala ya kuangalia matakwa yao na taifa kwa ujumla. .
.Mwito huo metolewa na Afisa
tarafa wa kata ya mikumi Godfrey Mwihumbo wakati
akifungua mkutano wa ukusanyaji wa maoni ya rasimu ya katiba mpya ulioandaliwa
na shirika la greenbelt trust fund kwa ufadhili wa fundition forcivil
socity katika kata ya Ruhembe na Ruaha
wilayani kilosa mkoani Morogoro
Mwihumbo alisema kuwa endapo
wananchi watashiriki kikamilifu kutoa maoni yao bila kutumiwa na kundi lolote
taifa litapata katiba yenye muongozo wenye manufaa kwa taifa na siyo bora
katiba .
Kwa upande wao washiriki walio
shiriki mkutano huo Thomas Mamleko na Lilian Jacob walisema kuwa
kuongezeka kwa serikali tatu ni kulisababishia taifa hasara kwani itatakiwa
kila serikali iwe na majeti yake .
Walisema kuwa kuwana serikali zaidi
ya mmoja kuna uwezekano mkubwa wa kuvunja amani ya nchi na pia uaminifu wa
vitega uchumi vitatakiwa kugawana ambapo kutasababisha taifa kuwa masikini.
Hivyo hivyo waliutaka uongozi unao
kusanya maoni ya rasimu kupitia mwenyekiti wake kutilia maanani suala zima la
ukusanyaji maoni na kuchukua yale ambayo yenye tija ya kulenga taifa nasiyo
kubomoa taifa na kusababisha taifa kuwa masikini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment