JESHI la polisi mkoani Morogoro kwa kushirkiana na Askari wa
hifadhi ya Udzungwa wanawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na
meno 10 ya tembo yenye thamani ya
shilingi mil.39.3 wakiwa tayari kusafirisha
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa morogoro,Faustine Shilogile
alisema kuwa mnamo tarehe 15/08/2013 katika eneo la Mzombe darajani mikumi
barabra ya Kilosa walipata taarifa kutoka kwa rai wema za kudai kuna gari
linapita likiwa tayatri na nyaraka hizo za serikali
Alisema polisi wa hifadhi walijipanga na kuweka doria katika
eneo hilo na ilopofika majira ya saa 5 usiku walikamata gari lenye namba za
usajili T.199 AQP aina ya fuso,na mara walipofanya upekuzi katika gari hilo
walikuta meno ya tembo 10 ikiwa kweny mfuko wa salfeti na kuchanganywa katika magnia ya
mchele
Kamanda alisema kuwa
kartika tukio hilo wanawashikilia watu wawili,pamoja na gari walilokuwa
wamebakia meno hayo na jeshi la pilisi linaendelea na upepelezi kuhusiana na
tukio hilo na utakapokamilika watuhumiwa wataplekwa mahakani kujibu shitaka
linalowakabili
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo
vya usalama katika kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu wowote unaotokea ndani
ya mkoa na zawadi nono zitatolewa kwa wale wanaotoa taarifa pamoja na
kutowataja ni nani katoa taarifa hiyo kwa sababu za kiusalama
Kwa upnde wake Mhifadhi Mkuu,hifadhi ya Milima ya
Udzungwa,Nitalis Uruka alisema kuwa meno hayo ya tembo yaliyokamatwa kwa
ushirikiano wa rai ni tembo 5 waliuliwa wenye thamani ya shilingi mil.120 jambo
ambalo ni hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania
Uruka alisema kuwa
wahalifu katika mbuga za wanyama wapo wengi sana hivyo jamii itambue
kuwa sio jambo zuri kuharibu mali asili za nchi kwa nia yeyote na atayehusika
katika hilo na kukamatwa atachukuliwa adhabu kali za kisheria iwe fundisho kwa
wengine wenye tabia kama hizo
Mhifadhi Mkuu wa Kanda,Fustine Masalu alisema kuwa wahujumu
wa uchumi walikamatwa huwa wanaua wanyama hao kwa siri na kutokana na biashara
hiyo hapa Tanzania haipo na kufanya mipango ya kupeleka katika nchi za jirani
zenye kuhitaji bidhaa hizo
Masalu alisema kuwa meno hiyo inaoenekana uharibifu
umefanyika kwa muda siku nyingi zaidi ya miezi 4 kuendelea mapaka hata miaka
3,na pindi wanapopata mwaya wa
kusafirisha ndipo wanatumia njia hizo kusafirisha mapa kwa wateja wao.
Kimath-Morogoro
No comments:
Post a Comment