Monday, July 15, 2013

VIONGOZI WA KIJIJI WASHUTUMIWA KUUZA ARDHI KINYEMELA.

WANANCHI zaidi ya 300 wa kijiji cha wami dakawa wamelalamikia uongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa kuuza mashamba yao yaliyopo katika kitongoji cha mkole yenye ukubwa wa hekari 280 bila kupewa taarifa na kufuata sheria na taratibu zilizopo

Wakulima na wafugaji hao walidai kuwa eneo hilo aliuziwa mwekezaji Amir Mohamed mara baada ya kununua  hekari 500 kwa mara ya kwanza kwa kufuata utaratibu sheria

Wakizungumza na waandishi wa habari katika mashamba ya mkole kijiji cha wami dakawa mkoani morogoro  baada ya kukagua mipaka iliyowekwa na mnunuzi wa mashamba hayo walidai kutotendewa haki hasa baada ya kuchukuliwa kwa maeneo yao  bila kupewa taarifa yoyote.

Walisema kuwa wamefukuzwa katika maeneo yao na kutojua mahali pakwenda na hivyo kuitaka serikali kusikiliza kilio chao kwani mashamba hayo yanawasaidia kukidhi mahitaji yao ya muhimu ikiwa kula,kusomesha pamoja na kupata huduma za afya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Abdalah Mgaya amekubali kupokea malalamiko hayo ofisini kwake kutoka kwa wakulima hao ambapo amefafanua kuwa eneo halali la mmiliki wa mashamba hayo ni hekari 780.

Mgaya aliema kuwa  serikali ya kijiji imepata uthibisho kutoka baraza la ardhi na sio hekari 500 kama inavyojulikana na wakulima hao ambao hawana hati halali za umiliki wa maeneo hayo kwani waliohusika kuuza maeneo hayo wamefuata taratibu na sheria za matumizi ya ardhi.

Mvomero.

No comments:

Post a Comment